Njia Za Kubana Matumizi Ya Petroli

Petrolprices

Kama tunavyojua kuwa petroli sasa imevuka

mpaka bila ya kutegemea kwa kipindi kidogo tu hadi kufikia £1.24 kwa lita

moja na bei hiyo inategemewa kufikia £1.40 kwa lita ifikapo pasaka ya mwaka huu.

Kutokana na hali inavyokwenda, inasemekana kwenye bajeti ya mwezi April mwaka huu inategemewa bei ya mafuta itapanda tena juu ya bei iliyopo hivi sasa, kwahivyo, kaeni mkao wa kula.

Hali hii imemkumba kila mtu ambaye

anategemea usafiri wa gari

SJ Post, imekusanya habari

kutoka sehemu tofauti za kuaminika, kutafuta njia za kukusaidia kukata matumizi yako ya petroli.

Njia gani unaweza kuzichukua

ambazo zitakusaidia kubana matumizi ya mafuta?

TAFUTA TOFAUTI YA BEI:

Kwanza kabisa, angalia eneo unalokaa kuna

stesheni ngapi za petroli ambazo unazijua na kabla haujatia petroli

zunguka stesheni zote za eneo lako kuangalia bei nafuu. Kwa kufanya hivi

itakusaidia kubana pesa. Chini ya maelezo haya, tumekuwekea kubonyeza

link ya mtandao hapo chini wa kukuwezesha wewe kutia Post Code ya eneo lako

kujua stesheni zote za karibu yako unapoishi na bei zake bila ya wewe kutoka nje na kutafuta bei za mafuta.

Mtandao huo utakupa tofauti ya bei zote za

stesheni za sehemu unayoishi (up to date) bei ghali na bei ya chini. Bei

za kila eneo hutofautiana kutoka 2p mpaka 15p kwa lita moja ambayo ikiwa unajaza

tenki la petroli la lita 40 unaweza ukasevu mpaka £6.00 kwa tenki moja la gari.

ENDESHA GARI KIMAKINIFU:

Tumia muda mrefu kuendesha gari kwa

kutumia gea ndogo (gea namba 5). Unapoondoa gari, usitumie muda mrefu

kuvuta kwenye gea kubwa (gea namba 1, 2, 3 na 4) gea namba hizi hutumia

mafuta mengi, kwa maana, ukitumia gea namba 3 kwenye mwendo wa 37mph

inakunywa asilimia 25% ya mafuta zaidi kuliko ukiwa unatumia gea namba 5

kwenye mwendo huo huo.

Vilevile unapokwenda safari ya mbali au

safari yenye magari mengi, pendelea kusikiliza habari za TRAFFIC za

redioni za kwenye gari kama LBC 97.3 au BBC 94.9 FM Radio ambayo huleta habari za TRAFFIC

kila baada ya dakika 15. Kufanya hivi, kutakusaidia kuepukana na njia

zenye magari mengi au njia iliyo na ajali ambayo itakusababisha wewe

kukaa kwenye foleni ya magari kwa kipindi kirefu.

TAFUTA NJIA TOFAUTI ZA USAFIRI:

Jaribu kutafuta njia tofauti za usafiri

ili kubana matumizi na kusevu matumizi ya petroli ya gari yako. Mfano,

tafuta rafiki au mfanyakazi mwenzio ambaye mnafanya wote kazi pamoja

kwenda kazini na gari moja lakini kuchangiana pesa za petroli badala ya

wewe kulipa pesa zote peke yako.

Jaribu kutumia usafiri wa umma kama basi

au treni (ikiwa miundombinu ya basi kuelekea unapokwenda ni mizuri) badala ya kutumia usafiri binafsi. Jaribu kutumia baiskeli ambayo

itakusaidia kubana matumizi ya petroli na vilevile itakufanya uwe na

afya nzuri.

Vilevile inapendekezwa kama unafikiria

kununua gari mpya, basi fikiria kununua "Green Car" ambazo

zinatumia umeme au (Electric, Hybrid, Hydrogen and Solar cars). Kwa hapa

UK, gari hizo zinasaidia kukata gharama ya TAX na vilevile

inasaidia kukata gharama ya petroli.

Inasemekana kuwa, robo ya magari ambayo

yapo UK hutumiwa kutembelewa na safari zisizozidi maili 2 (2 miles)

ambazo safari hizo zingeweza kutumiwa kwa njia ya mguu au (kutembea kwa

mguu).

Bonyeza mtandao ufuatao kujisajili (inachukua dakika tatu tu) na kuangalia bei za

petroli zilizopo karibu na maeneo unayoishi:

www.petrolprices.com

Advertisements