Membe Aona Mbali Kwa Kuhimiza Uraia Wa Nchi Mbili Kuingizwa Kwenye Rasimu Ya Katiba

Waziri Membe akiwasilisha mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba hoja ya kupendekeza uraia wa nchi mbili kuingizwa kwenye rasimu ya Katiba.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Joseph Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Jaji Augustine Ramadhan.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuujulisha Umma kuwa jana tarehe 26 Agosti, 2013, Mheshimiwa Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikutana na Uongozi wa Tume ya Marekebisho ya Katiba. Lengo la kukutana na Tume ilikuwa ni kuwasilisha pendekezo la haki ya Uraia wa nchi mbili kutamkwa na kutambuliwa kwenye Katiba mpya.

Mheshimiwa Waziri alikutana na Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Augustino Ramadhani, Makamu Mwenyekiti wa Tume pamoja na Katibu wa Tume na Naibu Katibu wa Tume.

Akiwasilisha hoja yake mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba, Mheshimiwa Waziri alisema yafuatayo:-
1. Suala la Uraia wa Nchi mbili haliko kwenye rasimu ya sasa iliyotolewa. Lengo la kufika Tume ni ni kuomba suala hilo liingizwe kwenye rasimu.

2. Amependekeza Katiba itamke kwamba, Raia wa Tanzania aliyeko nje hatafutiwa uraia wake na mtu yeyote, chombo chochote sheria au Katiba, eti tu kwa sababu raia huyo amechukua uraia nje ya nchi.

3. Katiba ikitamka hivyo, itungwe Sheria itakayofafanua haki, wajibu na masharti ya Mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili.

4. Katika kujenga hoja hizo tatu, Tume ilielezwa faida zitakazopatikana kwa kuitambua na kuishirikisha jamii ya Watanzania waliopo ughaibuni (Diaspora). Tume pia iliondolewa wasiwasi juu ya madai kuwa uraia wa nchi mbili unahatarisha usalama wa taifa au utawafanya baadhi ya watu kupiga kura wakiwa nje. Tume iliambiwa kuwa Sheria za Uchaguzi hutawala upigaji kura kwa raia walio ndani na nje na hauwi holela. Kuhusu suala la usalama, Waziri alisisitiza kama ni mashaka, basi mashaka hayo yawe kwa wageni wanaoomba uraia nchini kuliko watanzania walioko nje.

Katika kumalizia, Mheshimiwa Waziri alisisitiza, “bado naamini watanzania walioko nje sio wasaliti, They are just smart citizens”.

IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

20130828-022952.jpg

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s