Swala Na Kufuatiwa Na Baraza La Eid-el-Hajj Zanzibar

zanzibar

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akiwapamoja na viongozi na wananchi mbalimbali katika Swala ya Idi –El-Hjji ilioswaliwa Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.
 
 

 Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
 Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idd -El-Hajj lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
 Waumini wanawake katika swala ya Idd
 Kinamama katika baraza la Iddi
 Rais wa Zanzibar Dkt  Mohamed Ali Shein  akiwa pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumalizika kwa Baraza la la Idi -El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimia  wananchi baada ya wala ya Idd –El-Hajj ilioswaliwa Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.
 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika baraza la Idd -El-Hajj lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
 Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
 Sehemu ya kinamama katika baraza la Idd
 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika baraza la Idi -El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
 
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar   16/01/2013
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameendelea kusisitiza hali ya Amani na kukemea Vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Watu wachache wenye lengo la kuiharibu sifa ya Zanzibar.
Amesema tangu Karne zilizopita Zanzibar pamekuwa pahala pa Amani na utulivu na hivyo kuitaka jamii kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuwafichua watu ambao wanaoharibu Amani iliyopo.
Rais Shein ameyasema hayo leo katika Hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd lililofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kiujumla hali ya Amani na Utulivu imetanda kote katika Visiwa vya Zanzibar hali inayopelekea Serikali kupanga na kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo kwa lengo la kuimarisha uchumi na ustawi wa Wananchi wake.
Hata hivyo amekea tabia inayofanywa na baadhi ya Watu wachache wanaowahujumu na kuwatia hofu Wananchi pamoja na Wageni wanaoitembelea Zanzibar.
Amefahamisha kuwa hakuna Dini inayowaelekeza waumini wake kuwahujumu Wanadamu wengine na kwamba watakaobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amewahahakikishia Wananchi na Wageni kwamba vyombo vya Ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri ya kusimamia ulinzi na Usalama na kuitaka jamii kutoa ushirikiano unaohitajika.
 
Aidha Dkt. Shein amebainisha kuwa kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama na amani Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kiwango cha kuridhisha kutoka Asilimia 6.7 kwa mwaka 2011 hadi Asilimia 7.0 mwaka 2012.
Ameongeza kuwa hali hiyo inatoa matumaini makubwa hasa ikizingatiwa kuwa ukuaji wa uchumi katika Bara la Afrika ni Asilimia 5.3  ambapo kwa upande wa Ukuaji wa uchumi wa Dunia ni Asilimia 2.9
Kuhusu Zao la Karafuu Dkt. Shein amesema kuwa Shirika la Biashara la Taifa ZSTC linatarajia kununua tani 4,016 kwa mwaka 2013 na kuwaomba Wananchi waendelee kushirikiana na Serikali katika kupambana na watu wanaofanya Magendo ya Karafuu.
 
Awali Akimkaribisha Rais Shein kutoa Hotuba yake Waziri wa Katiba na Sheria Aboubakar Khamis Bakary alisema Serikali imepanga Sala na Baraza la Idd katika Siku kuu zote za IDD-EL HAJJ zitakuwa zikifanywa kitaifa katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo kwa mara hii Swala ya Idd ilifanyika kijiji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Unguja.
 
alifahamisha kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo ili Wananchi wa Mikoa yote ya Unguja na Pemba wapate fursa ya kuswali pamoja na Viongozi wao Wakuu wa Kiserikali lakini kwa upande wa Swala ya IDD EL-FITRI itaendelea kuswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Sherehe ya IDD EL HAJJ inakuja kila mwaka kufuatia kumalizika kwa Ibada ya Hijja inayofanyika MAKKA Nchini Saudia kwa Waislamu wenye uwezo wa kufanya Ibada hiyo.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  16/01/2013
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s