Mashindano Ya Kitaifa Ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu 2014 – Aisha Sururu Foundation

20140711-163218-59538839.jpg

MASAHIHISHO YA TAREHE: MASHINDANO YATAFANYIKA JUMAPILI TAREHE 13/07/2014 NA SI JUMAMOSI TAREHE 12/07/2014. SAMAHANINI KWA USUMBUFU.

Aisha Sururu Foundation inawataarifu fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur’an takatifu ya kitaifa ya mwaka 2014 yatafanyika Jumapili hii ya tarehe 13/07/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambapo vijana wanawake na waume walioshiriki katika mashindano hayo watapigania nafasi zao za kwanza mbele ya umma na wageni waalikwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 9 ya Tanzania ikiwemo visiwa vya Zanzibar na Pemba ambapo vijana watakaoshiriki kutoka visiwa vya Pemba ni vijana walemavu wa macho, walemavu wa viungo na kadhalika. Njoo uje ushuhudie uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu) vipi walemavu wa macho na vijana wengineo walivyojiwezesha kufika kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur’an ya kitaifa ya mwaka 2014.

Uongozi wa Aisha Sururu Foundation unawaalika Watanzania wote waje pamoja kushuhudia mashindano haya na kuwashajiisha vijana wote walioshiriki katika mashindano haya ya kitaifa ya mwaka 2014.

Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall

Tarehe 13/07/2014, Jumapili

Kuanzia saa tatu asubuhi (9am) mpaka saa nane mchana (2pm)
Wabillahi tawfeeq,

Ramadhan Mubaarak,

Ahsanteni.

20140711-163259-59579148.jpg

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s