Mashindano Ya Qur’an Ya Taifa 2015 (1436 AH) – Tanzania

asf logo

Assalaam alaykum,

Aisha Sururu Foundation inawataarifu fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur’an takatifu ya kitaifa ya mwaka 2015 (1436 AH) yatafanyika Jumapili hii ya tarehe 05/07/2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambapo vijana wanawake na waume walioshiriki katika mashindano hayo watapigania nafasi zao za kwanza mbele ya umma na wageni waalikwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 11 ya Tanzania ikiwemo visiwa vya Zanzibar na Pemba. Baadhi ya vijana washindanao kutoka Bukoba ni vijana walemavu wa macho. Njoo uje ushuhudie uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu) vipi walemavu wa macho na vijana wengineo walivyojiwezesha kufika kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur’an ya kitaifa ya mwaka 2015.

Uongozi wa Aisha Sururu Foundation unawaalika Watanzania wote waje pamoja kushuhudia mashindano haya na kuwashajiisha vijana wote walioshiriki katika mashindano haya ya kitaifa ya mwaka 2015.

Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall

Tarehe 05/07/2015, Jumapili

Kuanzia saa mbili asubuhi (8am) mpaka saa nane mchana (2pm)

Wageni rasmi waalikwa ni: Sheikh Othman Maalim, na, Mbunge wa wilaya ya Ilala mheshimiwa Mussa Azan (Zungu).

Wote mnakaribishwa.

Wabillahi tawfeeq,

Ramadhan Mubaarak.

Ahsanteni.

Aisha Sururu Foundation.

Advertisements

One thought on “Mashindano Ya Qur’an Ya Taifa 2015 (1436 AH) – Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s