Kisa Cha Mafundisho

Bwana mmoja kwa kujiona kwake aliingia kwenye restaurant, ile kuingia tu aligundua kulikuwa na kijana mmoja mwenye umri wa kama miaka 28 akiwa amekaa kwenye kona. Yule bwana alikwenda mpaka kaunta akatoa kitita cha pesa na kumrushia muhudumu kisha kwa sauti kubwa akasema “Muhudumu! namnunulia chakula kila mmoja aliemo humu ndani isipokuwa yule kijana pale konani”. Muhudumu alikusanya pesa na kuanza kugawa chakula cha bure kwa kila mtu aliyekuwemo ndani ya restaurant hiyo isipokuwa yule kijana mdogo. Yule kijana hakukasirika badala yake alimtazama yule bwana kisha kwa sauti kubwa akasema “ASANTE SANA”.

Yule bwana bila kujali kwa mara nyingine tena alivuta kitita cha pesa na kumtupia muhudumu kisha akapayuka “Sasa hivi nitamnunulia chupa ya soda na nyongeza ya chakula kila mtu aliyemo humu ndani isipokuwa yule mpuuzi aliyekaa pale kwenye kona.” Muhudumu kwa mara nyingine alikusanya ile pesa na kuanza kugawa chakula cha bure na soda kwa kila mtu aliyekuwemo mle ndani isipokuwa yule kijana. Baada ya muhudumu kukamilisha kuwahudumia kwa chakula na vinywaji yule kijana alimtazama yule bwana kisha akatabasam na kusema kwa mara nyingine “ASANTE SANA”.

Hii ilimshangaza yule bwana na kuamua kumuuliza muhudumu “Hivi yule kijana ana matatizo gani mbona nimenunua chakula na vinywaji kwa kila mtu aliyemo humu ndani isipokuwa yeye lakini hajachukia badala yake amekaa pale anatabasamu na kunishukuru eti “Asante sana!! Au ni chizi?”.

Muhudumu alitabasamu kisha akasema “hapana siyo chizi, bali yeye ndiye mmiliki wa hii restaurant hivyo anakushukuru kwa kuwa wewe ni mteja mzuri”.

Tabasam.

Rais Dkt Magufuli Aongoza Maadhimisho Ya Siku Ya Kumbukumbu Ya Mashujaa


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.


Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.


Shughuli za maadhimisho hayo ya siku ya Mashujaa zilipokuwa zikiendelea ndani ya uwanja huo wa Mashujaa.


Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa madhimisho ya siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi waliojitokeza kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHIMIZA MAKAO MAKUU KUHAMIA DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao.Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.

Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.

“Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.

“Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa” Amesema Rais Magufuli.

Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

SIKU YA MASHUJAA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wakati wa sherehe za kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita hapa nchini.

RAIS MAGUFULI AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI TAREHE 23 JULAI 2016


 Vilevile, Jumamosi ya tarehe 23 Julai 2016, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio zipatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharibika.

Kauli Ya Paul Makonda Kuhusu Ujumbe Uliowekwa Kwenye Mitandao Ya Kijamii 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumzia kwenye kipindi cha Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza akaunti bandia za mitandao mbalimbali kupitia jina lake amesema:

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inanza na cheo changu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda sio vingine hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo.” 

Anasema agizo lililowekwa katika mitandao ya kijami kuwa wananchi wasiokuwa na kazi watakwenda jela, ni batili na siyo la akaunti yake bali yeye ameagiza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayokaa.

Anataja kuwa kutokana na matatizo yaliyopo kamwe hataacha kupambana na mafisadi katika Halmashauri zote tatu, wauza dawa za kulevya “unga”, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.


Hivyo aliwataka:

wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa makini na kufuata maelekezo ya wenyeviti wa mitaa ambayo nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Akizungumzia ajira, alisema kuna mpango wa kuwachukua vijana zaidi ya 1,200 ambapo watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali ambao watapatikana kwa uchambuzi maalum.

“Tuna mkakati wa kuwachukua vijana zaidi ya 1,200 kwa ajili ya kuwapeleka katika mafunzo ya ujasiriamali, lakini ni lazima tuwatambue kwanza watu hao,” alisema.

Alidokeza kuwa kuna mpango wa kupanua muda wa kufanya biashara jijini tangu asubuhi hadi saa nne za usiku ili kuwapatia watu huduma kwa muda mrefu na kwamba kilichotakiwa ni kuimarishwa kwa usalama ikiwa ni pamoja na kuongeza taa sehemu mbalimbali za jiji.

Mambo mengine aliyozungumzia ni dhamira ya kuwawezesha walimu wa mkoani kwake waanze kusafiri bure katika mabasi ya mwendo kasi na kutowapa pesa ombaomba mitaani ili kuwafanya waondoke jijini.

Kuhusu maovu mbalimbali yanayofanyika jijini, Makonda alishutumu ushoga, utapeli na uvutaji wa madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na shisha.

“Ushoga umepingwa na vitabu vya dini na hakuna sheria inayoruhusu ushoga, kwa hili najua watu watanitukana sana lakini nguvu niliyo nayo hakuna wa kunisimamisha,” 

alisisitiza huku akiwaonya watu wanaojiingiza katika utapeli kwa kutumia majina ya watu wengine, likiwemo jina lake. 

Long sighted for the Ummah (public benefit). Alhamdulillah.