Mheshimiwa Paul Makonda Aenda Mbali Zaidi Kutekeleza Alichokiahidi BAKWATA

Kauli ya ufafanuzi ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, kwa Waislam juu ya ujenzi wa jengo jipya la BAKWATA jijini Dar es Salaam.

Kauli ya ufafanuzi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda, kwa Watanzania kwa ujumla juu ya ujenzi wa jengo jipya la BAKWATA jijini Dar es Salaam.

KWA UFUPI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda, katika hotuba yake ya siku ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la BAKWATA jijini Dar es Salaam, amelenga kusisitiza mchango mkubwa unaofanywa na viongozi wa dini katika nchi yetu, basi haina budi kuwawekea mazingira mazuri ili waweze kutekeleza kazi zao vyema katika jamii, na akasisitiza kwa kusema ataendelea kushirikiana kwa kuwasaidia viongozi wa dini bila ya kusikiliza yanayosemwa vipembeni.

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, katika hotuba yake ya siku ya kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la BAKWATA jijini Dar es Salaam, amelenga kusisitiza kwa Waislamu wote kuwa wamoja na kushikamana katika mambo yanayoleta tija zenye faida katika Uislam na akatolea mifano mbalimbali ambayo inawafik hoja ya ujenzi huo kwa dalili za aya za Qur’an na Hadith za Mtume Muhammad (S.A.W) na kuhimiza Waislam wasikae pembeni bali wawe mbele kwenye kutekeleza kwenye mambo ya kuujenga Uislam na siyo kukaa vipembeni na kuonyesha vidole. Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zubeir amesisitiza, pamoja na kuwa kuna baadhi ya watu wana shaka na mchango huo kutolewa kwa njia moja au nyingine na mtu ambaye si Muislam, Mufti Mkuu amewatoa khofu Waislam na wasiokuwa Waislam kwamba mchango huo unafaa baada ya kuangalia pande zote za Sharia, na amegusia kwamba Mheshimiwa Paul Makonda ana nafasi kubwa katika jamii yetu basi si vibaya ikiwa atajitolea mchango wake popote pale anapoona ana uwezo napo kwa nafasi yake. Na mheshimiwa Makonda alisadikisha hilo.

MWISHO WA UFUPI

Kwa kumalizia, hakuna kitu ambacho kikatokea chenye ikhtilaf baina ya mwanadamu kwa mwanadamu, au ikhtilaf baina ya watu mbalimbali wa itikadi zozote zile bila ya kuwa na suluhisho la watu kukaa pamoja na kuheshimiana tofauti zao na kutatua matatizo yao kwenye kila maeneo ya kimaisha.

Na mahsusi kwa hili suala la jengo la BAKWATA kwa maneno yaliyojitokeza kutoka kwa baadhi ya watu kuwa na dhana mbaya kwa viongozi wetu wa dini, hatuna budi tuwakumbushe kwamba Qur’an tukufu inatufundisha kihikma kwamba tunaweza kushirikiana pamoja ili kujenga lengo lolote tarajiwa, mfano Biashara, Amani, Upendo katika jamii na vyote vyenye kumpendeza Mwenyezi Mungu katika mambo mbalimbali ya kimaisha kwa kushirikiana pamoja lakini bila ya kuvuka mipaka ya kiitikadi, iwe ya kisiasa au ya kidini. Pamoja inawezekana bila ya kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Mbali na kisiasa au kiserikali, iwapo Waislam wanaohoji au watakaohoji hoja ya ushirikiano wa hili (jengo) lenye kuhusu kidini, waangalie Qur’an inavyosema:

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.

Qur’an (3:64)

Kwa hili la kidini, tunaishukuru serikali kwa kupitia uongozi wa Mheshimiwa Paul Makonda kwa kutimiza wajibu wake kihekima na kikatiba. Kuna tofauti kubwa baina ya elimu na hekima, elimu huja kwa njia zote za kusoma, za kuona, za kuhisi na za kusikia, lakini hekima ni kufanya maamuzi sahihi ya hali halisi ilivyo kwa kusikiliza hoja za pande zote kwa umakini na kuleta tija kwa lengo tarajiwa na hata mara nyingine mpaka matokeo yake kupelekea hekima kuishinda elimu. Kwa hilo pia tunawashukuru viongozi wetu wa dini kwa hekima walioichukua kutokana na elimu waliyonayo katika suala hili zima.

Mungu ibariki Tanzania, Watu wake na Viongozi wake. Amin.

Samahani kama nimekosea popote.

Ndugu yenu,

Saleh Jaber.

28/08/2016

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s