TANZANIA MBELE: CHINI YA MWAKA MMOJA MAGUFULI NA KASI YA VIOJA

  • Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli afanya makubwa kabla ya kutimiza kilele cha mwaka mmoja tangu achukue ofisi ya Urais

  • Hotuba kamili ya Rais John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa ndege mpya za kisasa FAHARI YA TANZANIA

  • Azungumzia utendaji kazi wa Air Tanzania mpya

  • Azungumzia ubora wa ndege hizo na mtazamo wa huduma zake

 

 

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli afungua rasmi mradi wa usafiri wa anga AIR TANZANIA mpya, kwa kununua ndege mpya mbili kwa pesa taslimu.

Mheshimiwa Rais amewaomba Watanzania watumie ndege hizi kwa safari zao zote za ndani ya nchi bara na visiwani (domestic flights) ziwe safari za kibiashara, kistarehe au kutembelea familia zao, na hata pale ndege hizo zitakapoenda katika nchi za jirani (international or long haul flights) ili kuchochea uchumi wa taifa na hatimaye wafaidika watakuwa ni Watanzania wenyewe.

Mheshimiwa Rais ameahidi kununa ndege nyingine kubwa mbili ambazo zitakazofanya safari za kupasua anga za kimataifa ndani na nje ya Afrika na kuwa ni chachu ya kukuza shirika la ndege la taifa Air Tanzania kujizaa upya na kuwa na ndege nyingine zaidi ya kumi.

Pongezi kwa Rais wetu, tunajivuna na tunakupongeza Rais wetu kwa kuonyesha shauku na kuwa na ari ya uzalendo ya kuinua taifa letu na watu wake kwenye anga za kimataifa. Umeonyesha vioja ndani ya mwaka mmoja ambao wengi hawakutegemea kuwa wanayoyaona kuwa yatakuwa. Umejenga, umeendeleza na umezinduwa madaraja na barabara kwa viwango bila ya kuripuwa. Mwenyezi Mungu akulinde na akuzidishie afya, hekima na kila jema ulitakalo kuwa litakuwa. Amin.

ndani-ya-ndege

Ndani ya ndege, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada ya kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam, tarehe 28 Septemba 2016.

Advertisements

RC MAKONDA APONGEZA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

UONGOZI UNAOACHA ALAMA

Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, mheshimiwa Paul Makonda kwa majukumu yake ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ametoa siku mbili za huduma bure ya afya (AFYA CHECK) Jumamosi na Jumapili iliyopita kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa wale ambao hawana viashiria vyovyote vya magonjwa na kwa wale ambao wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Zoezi hilo limelenga wakazi wa Dar es Salaam ambao wenye uwezo wa chini na wote kwa ujumla.

Kutokana na uadimu na umuhimu wa zoezi hilo, lilivutia wakazi wengi wa Dar es Salaam na hata wa miji mingine ambayo iliyopo nje kidogo ya Dar es Salaam kuja kupata huduma hiyo. Mkuu wa Mkoa mheshimiwa Paul Makonda alisema wameshtukizwa na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwenye zoezi hilo ambalo limebaini umuhimu wa zoezi hilo kufanyika wakati muwafaka na kuagiza siku mbili nyingine ziongezwe Jumatatu na Jumanne iliyopita, ili ziweze kukidhi haja za wakazi waliohudhuria kwa kupatiwa huduma stahiki.

Zoezi hili ni zoezi linalopaswa pongezi sana kwasababu inasemekana katika watu waliohudhuria tu peke yake, asilimia 90 kati ya watu hao wamegundulikana na magonjwa mbalimbali.

Aidha, mbali na zahanati na hospitali za Kiserikali, kuna umuhimu wa taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini za Kiislam na za Kikristo kufungua huduma hizi kwa bei ya chini au hata ikiwezekana kuwa bure ili ziweze kuhudumia watu mbalimbali bila ya kuwa na vigezo au vizuizi ambavyo vitamfanya mkazi wa mkoa wowote kwenda kupata matibabu stahiki. Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa mheshimiwa Paul Makonda kwa kuliona hili.

Ndege Mpya Zote Mbili Zimeshawasili Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho (leo) anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho (leo) kuanzia saa mbili asubuhi.

“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.

Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MIGOGORO KATIKA MIRATHI – PART 1 & 2

Mchango wa kielimu wa kuijenga jamii kiAmani hususan wale walengwa wa mada, Waislam, na hata kwa jamii yote kwa ujumla. Mchango huu umetolewa na Sheikh Mohammed Bu-E’id na Sheikh Khamis Mataka (pichani juu).

MTAZAMO KWA UFUPI:

Mtazamo wa athari katika jamii jinsi inavyoweza kuathirika na kuleta migogoro na migongano juu ya suala la Mirathi na Sharia nyingine za kidini pale sharia za kidini ambazo ni sharia za Mwenyezi Mungu zinapoendeshwa kinyume na sharia zenyewe zilivyo.

Mlango wa sharia ni mlango mpana sana na baadhi za sharia haziangaliwi kwa athari ya hoja moja tu, kwasababu hoja hubadilika kutokana na mazingira, lakini sharia za Mwenyezi Mungu zimelenga mazingira yote kwa ujumla na usuluhisho wake upo wazi kisharia. Kwa mfano, vipi tunaweza kumsaidia au kumuhukumu mwanamke ambaye anajiuza barabarani kwa madai ya kujitafutia rizki yake ya kimaisha, ambapo kufanya hivyo ni kujihatarishia maisha yake na pia kuwa na nafasi kubwa ya kuambukizwa kwa maradhi mbalimbali yanayo sababishwa na ngono na kupelekea kuathiri jamii kwa ujumla na watu wake wa karibu waliyomzunguka. Je, tumsaidie kiuchumi kwa kumuwezesha na kujitegemea? Atafute au tumtafutie mume wa kuweza kuishi nae kumuondoa kwenye hali hiyo ya kufedheheka kwa mwanamke? Sharia za kidini zina majibu ya masuali yote haya! Na tunaishukuru serikali kwa kuipa heshima katiba yetu ya Tanzania kwa kuzipa uhuru dini bila ya kuingilia misingi ya Sharia ya kidini kwa mfano hii sharia ya Mirathi kwa wahusika kuwa huru na uamuzi wao wa kidini.

Hakuna sababu ya kupiga vita kitu kizuri chenye kujenga jamii ya Amani. Kukijenga kilichojengwa ni kukibomoa!

Swala Ya Eid-el-Hajj Dar es Salaam

eid5

Sheikh Abdulqadir Mohamed akiongoza swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid3

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa alijumuika na waumini wengine wa Kiislam katika swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid2

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisikiliza khutba na waumini wengine wa Kiislam katika swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

TUMIENI NYUMBA ZA IBADA KUHAMASISHA AMANI – WAZIRI MKUU MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA

eid6

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini zote  kutumia nyumba za ibada kuwahamasisha waumini wao umuhimu wa kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini. Amesema Serikali itahakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini ili Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato na kuwaletea tija.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumatatu, Septemba 12, 2016) wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Haji kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam.

“Serikali itaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote nchini. Wito wangu kwa viongozi wa dini msisitize waumini juu ya utunzaji wa amani pamoja na kukemea vitendo viovu ili Taifa lizidi kusonga mbele,” amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi kuendelea kuwaombea mahujaji waliopo mjini Makka na Madina nchini Saudi Arabia wakiendelea na ibada ya hijja warudi salama.Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwasaidia kwa hali na mali watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambako jumla ya watu 16 walifariki na wengine 253 kujeruhiwa.

Pia maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.Awali akisoma hutuba ya Eid viwanjani hapo Sheikh Nurdin Kishki alisema dini ya Uislamu ni dini ya amani hivyo amewaomba waislamu kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani yakiwemo mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Sheikh Kishki amesema ni muhimu watu kulinda amani kwani ikitoweka ni vigumu kuirudisha, alitolea mfano wanachi wa nchi za  Libya na Misri ambazo hadi sasa zimeshindwa kuirudisha. Amesema mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya uwamwagaji wa damu, kudhulumu mali za watu pamoja na kuwavunjia heshima wenzake atakuwa ameangamia, hivyo amewataka Watanzania hususan wakazi wa Temeke kujiepusha navyo.

“Temeke sasa inaongoza kwa matukio ya mauaji, wanaua hadi walinzi. Askari wameuawa bila hatia, jambo hili linasikitisha sana. Watu waliokuwa wanafanya kazi ya kulinda raia na mali zao wanauawa bila ya hatia! Ameongea kwa masikitiko na kuwaomba Watanzania wajiepushe na vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine Sheikh Kishki ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo hivyo amewaomba wananchi wawe mstari wa mbele kutoa ushirikiano ili taifa liweze kusomba mbele.

“Ndugu zangu tumepewa heshima kubwa leo kuswali Eid na Mheshimiwa Waziri Mkuu tena amekuja hapa kwenye viwanja hivi vya Mwembe Yanga, hii inaonyesha ukaribu wa viongozi wetu wakuu kwa wananchi wao hususan wa hali ya chini,” amesema.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P. 3021,

11410 DAR ES SALAAM.

JUMATATU SEPTEMBA  12, 2016

eid1

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akitoa khutba kwa waumini wa Kiislam katika swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid4

Waziri Mkuu Kassim Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Nurdin Kishki, wakiomba dua ya pamoja baada ya swala ya Eid-el-Hajj kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid7

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwaaga waumini wa Kiislam mara baada ya kumalizika kwa swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid8

eid9

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiwajulia hali wagonjwa wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki swala ya Eid-el-Hajj jana asubuhi.

eid10

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati alipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki swala ya Ei-el-Hajj jana asubuhi.

Swala Ya Eid-el-Hajj Dar es Salaam

eid9

Waumini wa dini ya Kiislam walijumuika kuswali swala ya Eid-el-Hajj iliyofanyika viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid7

Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisikiliza khutba ya swala ya Eid-el-Hajj iliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir na kushoto kwake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Musa Salum pamoja na waumini wengine wa Kiislam, jana asubuhi.

eid10.jpg

eid8

Baadhi ya waumini wa Kiislam wakisikiliza khutba ya swala ya Eid-el-Hajj iliyofanyika viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid2

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir akitoa khutba kwa waumini wa Kiislam baada ya kukamilika kwa swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

Sheikh Abubakar Zubeir amesema kuwa anawatakia Waislamu kote nchini na wananchi kwa jumla sikukuu njema ya Eid-el-Hajj ili kila mmoja aisherehekee kwa utulivu na mshikamano.

Amewataka pia waalimu kote nchini wa shule za Kiislamu za madrasa kufanya jitihada kubwa ya kuhakikisha wanawaelimisha wanafunzi wao ili waweze kuwa na maadili mema ya dini yao na akaongeza kuwa kazi yao si kuwapatia elimu ya dini yao tu, bali wafundishwe pia masomo mbalimbali na lugha za nchi nyingine ili kuwawezesha kuwa na maadili mema na utaalam unaotakiwa katika maisha yao ya baadaye na kuwa viongozi bora.

Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika khutba yake, amesisitiza suala la amani kwa Watanzania wote huku akikazia maneno ya Mufti Zubeir aliyokuwa ameyatamka ili waumini waweze kubadilika akimaanisha kuondokana na dhana zozote potofu zisizokuwa na manufaa katika kulijenga taifa.

eid1

Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akitoa khutba kwa waumini wa Kiislam baada ya kukamilika kwa swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid3

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Musa Salum akitoa khutba kwa waumini wa Kiislam baada ya kukamilika kwa swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid6

Kutoka kushoto ni Abdallah Bulembo akifuatiwa na aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Suleiman Kova pamoja na Sheikh Suleiman Lolila na waheshimiwa wengine na Masheikh wakubwa wakisikiliza khutba ya swala ya Eid-el-Hajj iliyofanyika viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid4

Mheshimiwa Ramadhan Madabida (wa pili kutoka kushoto) akifuatiwa na Mbunge wa Chalinze, Ridhwan Kikwete na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakisikiliza khutba ya swala ya Eid-el-Hajj iliyofanyika viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid11

Sheikh Ali Khamis Ngeruko, akitoa khutba kwa waumini wa Kiislam kwenye mjumuiko wa swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

WAISLAM WAASWA KUUNGA MKONO MABADILIKO YA BAKWATA

Waziri Mkuu Aongoza Wananchi Kuaga Miili Ya Waliokufa Kwa Tetemeko

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016) mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.

“Poleni sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu  Serikali ipo pamoja nanyi na haitawatupa mkono,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia waathirika.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo salama la kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.

Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.

Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, SEPTEMBA 11, 2016