Vijana Watakiwa Kuchangamkia Fursa Za Kiuchumi

BAKWATA yafungua rasmi baraza la vijana la Waislam jijini Dar es Salaam leo. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Musa Salum, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir na mgeni wa heshima mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Polisi mstaafu mheshimiwa Suleiman Kova, wamehimiza vijana kwa ujumla kuchangamkia fursa za kiuchumi kujipatia rizki halali na kuachana na mambo yoyote yanayoleta uchochezi mbaya.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli alimalizia ziara yake ya Zanzibar kisiwani Unguja leo, baada ya ziara yake ya kisiwani Pemba jana.

Katika hotuba yake kisiwani Unguja leo, Rais Magufuli aliendelea kusisitiza Amani, Upendo, Mshikamano kwa Watanzania wote bila ya kujali itikadi zao. Rais Magufuli aligusia baadhi ya maendeleo yaliyotekelezwa na serikali na mengi yatakayofunguka siku zijazo katika kuleta huduma za msingi na fursa za kiuchumi kwa kuwaletea Mapinduzi ya Viwanda kwa wananchi wa visiwani Zanzibar sambamba na dira ya taifa ya mwaka 2025.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s