Swala Ya Eid-el-Hajj Dar es Salaam

eid5

Sheikh Abdulqadir Mohamed akiongoza swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid3

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa alijumuika na waumini wengine wa Kiislam katika swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid2

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisikiliza khutba na waumini wengine wa Kiislam katika swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

TUMIENI NYUMBA ZA IBADA KUHAMASISHA AMANI – WAZIRI MKUU MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA

eid6

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini zote  kutumia nyumba za ibada kuwahamasisha waumini wao umuhimu wa kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini. Amesema Serikali itahakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini ili Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato na kuwaletea tija.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumatatu, Septemba 12, 2016) wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Haji kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam.

“Serikali itaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote nchini. Wito wangu kwa viongozi wa dini msisitize waumini juu ya utunzaji wa amani pamoja na kukemea vitendo viovu ili Taifa lizidi kusonga mbele,” amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi kuendelea kuwaombea mahujaji waliopo mjini Makka na Madina nchini Saudi Arabia wakiendelea na ibada ya hijja warudi salama.Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwasaidia kwa hali na mali watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambako jumla ya watu 16 walifariki na wengine 253 kujeruhiwa.

Pia maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.Awali akisoma hutuba ya Eid viwanjani hapo Sheikh Nurdin Kishki alisema dini ya Uislamu ni dini ya amani hivyo amewaomba waislamu kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani yakiwemo mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Sheikh Kishki amesema ni muhimu watu kulinda amani kwani ikitoweka ni vigumu kuirudisha, alitolea mfano wanachi wa nchi za  Libya na Misri ambazo hadi sasa zimeshindwa kuirudisha. Amesema mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya uwamwagaji wa damu, kudhulumu mali za watu pamoja na kuwavunjia heshima wenzake atakuwa ameangamia, hivyo amewataka Watanzania hususan wakazi wa Temeke kujiepusha navyo.

“Temeke sasa inaongoza kwa matukio ya mauaji, wanaua hadi walinzi. Askari wameuawa bila hatia, jambo hili linasikitisha sana. Watu waliokuwa wanafanya kazi ya kulinda raia na mali zao wanauawa bila ya hatia! Ameongea kwa masikitiko na kuwaomba Watanzania wajiepushe na vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine Sheikh Kishki ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo hivyo amewaomba wananchi wawe mstari wa mbele kutoa ushirikiano ili taifa liweze kusomba mbele.

“Ndugu zangu tumepewa heshima kubwa leo kuswali Eid na Mheshimiwa Waziri Mkuu tena amekuja hapa kwenye viwanja hivi vya Mwembe Yanga, hii inaonyesha ukaribu wa viongozi wetu wakuu kwa wananchi wao hususan wa hali ya chini,” amesema.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P. 3021,

11410 DAR ES SALAAM.

JUMATATU SEPTEMBA  12, 2016

eid1

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akitoa khutba kwa waumini wa Kiislam katika swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid4

Waziri Mkuu Kassim Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Nurdin Kishki, wakiomba dua ya pamoja baada ya swala ya Eid-el-Hajj kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid7

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwaaga waumini wa Kiislam mara baada ya kumalizika kwa swala ya Eid-el-Hajj iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

eid8

eid9

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiwajulia hali wagonjwa wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki swala ya Eid-el-Hajj jana asubuhi.

eid10

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati alipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki swala ya Ei-el-Hajj jana asubuhi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s