AMSONS GROUP YATIMIZA AHADI YAKE KWA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA NA KWA HESHIMA YA MAMA SAMIA SULUHU

  • Mradi wa upanuzi wa wodi za wazazi katika hospitali za wilaya tatu mahsusi za jijini Dar es Salaam, wilaya ya Ilala, Kinondoni na Temeke, zimewekewa mawe ya msingi kuashiria mwanzo wa ujenzi wa mradi huo.

  • Mkurugenzi wa kampuni ya AMSONS GROUP, Abdallah Nahdi, ambaye ndiye muwakilishi wa ufadhili wa mradi huo, amesema aliguswa kuona jinsi wanawake wajawazito na wanawake waliojifungua kuwemo katika mazingira mabaya ya ujauzito wao na kuamua kuwajengea mazingira mazuri

  • Amesema AMSONS GROUP haifanyi haya kwasababu yake binafsi bali ni kama mchango wake kwa jamii na kwa wananchi kwa ujumla, na anafahamu uzito wa mama mzazi katika jamii na aomba ushirikiano na wahusika katika kukamilisha miradi hiyo na dua kutoka kwa wananchi ili wakamilishe waliyoyakusudia

  • Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu alifungua hotuba yake kwa kumshukuru Mungu na kutoa dondoo za jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyojikita katika kufanikisha maendeleo kwa wananchi na aliwapa salamu kutoka kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa wote waliohudhuria hafla hiyo na wakazi wa wilaya zote kwa ujumla wazidi kumuombea Mungu ili afikie malengo yake kwa wananchi

  • Mheshimiwa Samia Suluhu asema changamoto ni nyingi na tupo kwenye wakati wa mabadiliko ya kimaendeleo na awaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani changamoto hizo ni za mpito

  • Makamu wa Waziri wa Afya, Mheshimiwa Khamis Kigwangala asema atahakikisha kupigana usiku na mchana kupunguza kwa kasi kubwa vifo vya wajawazito na vifo vyote vinavyotokana na uzazi

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah J. Kairuki amemuhakikishia Makamu wa Rais kuwa atasimamia na atatoa yote yatakayohitajika kutoka kwenye ofisi yake na kuhakikisha wodi hizo zinatoa huduma tarajiwa

  • Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Paul Makonda asema amefurahi kuwa mradi huo sasa unafanyika kimatendo na nia yake kubwa si kutumikia wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa faida yake binafsi, bali ni kwa kutumia nafasi yake aliyopewa na Mungu kutumikia wakazi wa Dar es Salaam, Kuwapa heshima waliompa nafasi hiyo ya uongozi wa jiji la Dar es Salaam na mwisho ni Kuwacha alama kwa jamii, amesema Paul Makonda

  • Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wote waliwashukuru wafadhili na wageni waheshimiwa kufika katika uwekaji wa jiwe la msingi la majengo ya wodi hizo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s