KUMBUKUMBU NA HEKIMA ZA MWALIMU JK NYERERE ZA KUJENGA UIMARA NA UMOJA WA TAIFA

  • Katika kongamano la kumuenzi baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Alhajj Ali Hassan Mwinyi amesema Jamii inatakiwa kumuenzi baba wa taifa kwa kujenga UMOJA WA KITAIFA

  • Mheshimiwa Alhajj Ali Hassan Mwinyi akiwa ni mzee mmojawapo kama hazina ya taifa amesema, uadilifu aliouwacha Mwalimu Nyerere kwa sasa umeporomoka, kwa hikma za mzee Alhajj Ali Hassan Mwinyi ametanguliza suali nani wakulaumiwa katika hili na ameita wito wa taifa zima kutafakari misingi iliyowachwa na Mwalimu Nyerere ya umoja wa kitaifa

  • Profesa Issa Shivji naye amewakosoa baadhi ya Wanasiasa wanaotumia dhana ya kizalendo kuchochea Ubaguzi, Udini, Ukanda na Ukabila na kwamba wakiachiwa watalichana taifa. Na huku baadhi ya wachangiaji walizungumzia urithi wa taifa kutoka kwa Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 17 iliyopita kuwa Uhuru, Umoja, Usawa, Kuheshimiana na Rasilimali taifa kutumika kwa faida ya wote

  • Joseph Kahama naye amekumbushia tunu ya Katiba yetu ya Tanzania na athari zake iwapo tutaichezea au iwapo itachezewa

  • Mheshimiwa Joseph Butiku naye amesisitiza Umoja, Usawa kwa watu wote, Wanaoheshimiana, Wenye uhuru, Heshima na Hadhi na Rasilimali taifa kutumika kwa faida ya wote

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s