-
Mfalme Mohammed VI wa Morocco ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti mkubwa jijini Dar es Salaam wenye uwezo wa kuchukuwa mpaka watu elfu sita kwa wakati mmoja
-
Msikiti huo ambao ni msaada kutoka falme ya Morocco, ni moja ya michango aliyoitowa Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kupitia maombi na jitihada za Rais Magufuli kwa niaba ya Waislamu wa Tanzania
-
Msikiti huo utakuwa na ofisi mbalimbali ikiwemo ofisi ya asasi ya Mfalme mwenyewe na ukumbi wa mikutano wa kimataifa
-
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema hii ni neema kubwa na amesisitiza Waislamu waendelee kuwa na umoja, kupendana na kushikamana
-
Mbali na msaada huo, Mfalme Mohammed VI wa Morocco ametoa Qur’an (misahafu) elfu kumi
-
Katika hafla hiyo walikuwapo wageni wa heshma mbalimbali akiwamo Alhajj Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Gharib Bilal, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda ambaye amewatakia Waislamu kila la kheri
Mfalme Mohammed wa Morocco VI akibusu Qur’an (Msahafu) kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir.
Advertisements