MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA MHESHIMIWA HAILEMARIAM DESALEGN KATIKA ZIARA YA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA BAINA YA NCHI MBILI

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, amempokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Hailemariam Desalegn, jijini Dar es Salaam ambaye atakaa siku mbili katika ziara yake ya kikazi

  • Tanzania na Ethiopia wametiliana saini katika mikataba takriban 15 katika maendeleo ya mawasiliano, utalii, umeme wa bei ya chini, madini, kilimo, mifugo, michezo, ulinzi na usalama, viwanda, kukuza lugha ya Kiswahili nchini Ethiopia na mengineyo mengi ikiwemo elimu ya anga na usafirishaji wa shehena kwa njia ya ndege ambao usafirishwaji huo unatarajiwa kitovu chake kuwa jijini Dar es Salaam na kuwa kitovu kikubwa cha usafirishaji wa shehena kwa njia ya ndege ndani ya Afrika

  • Aupongeza mtandao wa ndege za Ethiopia ambazo sasa zipo zaidi ya ndege mia moja katika mtandao wao wa usafirishaji, na kuna matarajio makubwa ya ushirikiano baina ya Ethiopian Airline na Air Tanzania katika utengenezaji wa ndege, mafunzo ya elimu ya anga na mabadilishano ya kiujuzi. Vilevile asifia huduma za ndani ya ndege za Ethiopia

  • Aipa nchi ya Ethiopia sifa stahili ya kutokutawaliwa na wakoloni, nchi ambayo ina historia kubwa ya kifalme na kimalkia ikiwamo historia ya Mfalme (Mtume) Suleiman na Malkia Sheba

  • Mheshimiwa Desalegn naye amesema amefarijika kwa ujio wake na amefurahishwa kwa mapokezi makarimu ya watu wa Tanzania, yeye pamoja na jopo lake

  • Amhakikishia Rais Magufuli na Watanzania kuendeleza ushirikiano baina ya nchi mbili kwa kuamini kuwa Tanzania na Ethiopia wana uhusiano wa kihistoria, kiutamaduni na kifikra pamoja na kuwepo kwa changamoto zinazofanana za kiuchumi na za kijamii ambazo ameomba kubadilishana fikra kwenye kutatua changamoto hizo

  • Asisitiza kwamba ni muhimu Afrika na watu wake wenyewe washirikiane katika kubadilishana ujuzi na fikra mbalimbali za kutatua changamoto hizo zinazokabili nchi zao, ama kwa nchi yake ameomba ushirikiano wa kutatua changamoto hizo hususan kutoka nchi ya Tanzania. Aamini kwamba ujuzi, fikra na uwezo wa watu wa nchi mbili hizi katika kipindi cha fursa iliyopo hivi sasa, unahitajika zaidi. Kipindi ambacho upepo wa uchumi wa dunia ambao ulielekea bara la Asia, sasa unaelekea bara la Afrika, amesema Mheshimiwa Desalegn

  • Amehimiza ushirikiano sana kwenye sekta ya kilimo kwa imani ya kwamba, kilimo ni njia mojawapo ya kuwatoa wananchi kwenye umaskini na kuwapa maisha bora. Amesihi ni muhimu kwa sasa kutumika kwa nguvu-kazi za wananchi, hususan vijana, kwenye kuleta maendeleo ya nchi kabla ya maendeleo ya teknolojia

  • Mwisho ameupongeza uongozi wa busara wa Rais Magufuli na amezitakia nchi zote mbili kuwa na uhusiano mwema na wa kudumu

Advertisements