MHESHIMIWA RIDHWAN KIKWETE MSAFI BAADA YA KAMISHNA NA KAMATI YA UCHUNGUZI KUJIRIDHISHA

ridhwan kikwete

Mbunge wa Chalinze, Mheshimiwa Ridhwan Kikwete asema ameshukuru kuitwa na Kamishna wa Kuzuia Madawa ya Kulevya, Mheshimiwa Rogers Sianga, kufanyiwa mahojiano kutokana na tuhuma za madawa ya kulevya. Ridhwan amesema, ni kheri kwake kufikiwa na hatua hiyo kwasababu suala hili lilishaanza kuleta taharuki katika jamii na kaona ni busara kuijulisha jamii kwamba hausiki na madawa ya kulevya au mikhadarati ya aina yoyote na kwahivyo ni msafi.

Mheshimiwa Ridhwan amesema, ilifika wakati hata baba yake alimwita kumuuliza kuhusu suala hili ili amuwekee wazi kuhusu ukweli wa mambo. Ridhwan alimwambia baba yake, hausiki kabisa na wala hajawahi kuhusika na suala la madawa ya kulevya hata siku moja katika maisha yake.

Mheshimiwa Ridhwan ameshauri kwamba madamu sasa chombo maalum cha serikali kimeshaundwa kushughulikia suala hili, ni bora chombo kimoja tu cha serikali kifanye kazi ili kusiwe na migongano ya kiutendaji ambayo inaweza kusababisha kuwagawa wananchi (na hata upotevu wa rasilimali za taifa).

Mwisho Ridhwan ameshukuru kwa upande wake kuwa hili jambo sasa limekwisha, na ameipongeza na kuunga mkono jitihada za serikali za kupigana na madawa ya kulevya na mikhadarati yote kwa ujumla zinazoendelea hivi sasa.

Msikilize kwa urefu hapa:

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s