BWANA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS AONGEA KWA UNYENYEKEVU MKUBWA KABISA KUTAKA USAWIYA WA TUKIO LA CLOUDS

ruge

KWA UFUPI:

Bwana Ruge Mutahaba wa kampuni ya Clouds, asikika katika kipindi cha redio ya Clouds akizungumza kwa unyenyekevu wa hali ya juu, juu ya tukio lililotokea kwenye viwanja vya Clouds na Mheshimiwa Paul Makonda.

Bwana Ruge amekuwa akisikika katika vyombo vya habari kuhusu tukio hilo, akidai kwamba, mbali na ushirikiano wa kikazi aliyokuwa nao na Mheshimiwa Paul Makonda, lakini Mheshimiwa Paul Makonda ni rafiki yake mkubwa na ataendelea kuwa rafiki yake.

Wakati huku wakingoja kauli ya Waziri wa Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye baada ya kuunda timu ya ufuatiliaji wa tukio la Clouds, Bwana Ruge amshauri Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Paul Makonda kusuluhishana nae ili kuleta usawiya juu ya tukio hilo, alisema Ruge huku akisikika kwa sauti ya chini na ya upole kabisa.

Mwisho, Ruge alisisitiza kwamba hoja hii siyo ya kumtaka Mkuu wa Mkoa kutumbuliwa, bali ni kutaka usawiya katika tukio lililotokea katika viwanja vya Clouds ambalo hakupendezewa nalo. Ruge alisikika mara kadhaa akisifu na kupongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote kwa ujumla na kwahivyo amesema ataendelea kuisaidia serikali katika kuzitangaza sera zake, na katika maendeleo ya Dar es Salaam na maendeleo ya mikoa mbalimbali nchini, kwasababu anaipenda Dar es Salaam na anaipenda Tanzania, amesema Ruge.

Advertisements