RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MRADI WA TRENI ZA KISASA (STANDARD GAUGE TRAINS)

  • “Kwahiyo niendelee?”, “Kwahiyo niendelee?”, “Kwahiyo niendelee?” Ni masuali matatu aliyoyauliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, kwa wananchi kwenye hotuba yake alipohudhuria uzinduzi wa mradi mpya wa treni za kisasa [(Standard Gauge Trains) zitakazotoka Dar es Salaam hadi Morogoro], uliofanyika Pugu, jijini Dar es Salaam. Jibu kutoka kwa wananchi lilikuwa “Endeleaaa”

  • Akiwa ndani ya mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu achukue ofisi ya urais, Rais Magufuli kafanya na kaonesha mengi ya kuiletea sifa nchi ya Tanzania na wananchi wake, mbali na mwendo wake wa kasi kufikia maendeleo tarajiwa, bali ni kwa kuzindua na kuifufua miradi mikubwa mikubwa kama shirika la ndege la taifa (ATCL) na mengineyo mengi, mmoja wapo ni mradi huu aliouzindua leo wa treni za kisasa kwa kutumia shilingi ya Tanzania taslimu bila ya kukopa na bila ya kutegemea msaada kutoka nje

  • Kwa kufanikisha hayo, mheshimiwa rais amewapongeza na kuwashukuru waheshimiwa wabunge kwa kupitisha matumizi ya pesa za mradi wa maendeleo ya treni za kisasa (miundombinu) ambazo zitaleta ajira kwa wakazi wa Pugu na maeneo mengine ya Tanzania, zitakuwa ni moja wapo ya chachu ya maendeleo ya taifa na zitakuwa moja wapo ya chachu ya kuchochea uchumi wa viwanda

  • Mwisho mheshimiwa rais aliwashukuru viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, na akawashukuru wananchi wote kwa kumuamini kuiongoza nchi na akawasisitiza kushikana pamoja katika maendeleo ya taifa. “Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki reli hii ya ‘standard gauge’, Mungu awabariki wana Pugu wote…”, alimalizia hotuba yake kwa kusema hayo

Advertisements