MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MABWENI YA CHUO KIKUU KATIKA KUTIMIZA AHADI YAKE ALIYOIWEKA

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, amehudhuria kwenye uzinduzi wa mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambayo ameyaasisi yeye baada ya kuona tatizo kubwa la makazi na malazi linalowakabili wanafunzi wa chuo hicho, chuo ambacho amekiita ndicho chuo kikuu mama katika historia ya Tanzania. Ujenzi huu ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa kwa wanafunzi, mwaka wa jana (2016)

  • Kabla ya kuanza hotuba yake, Mheshimiwa Magufuli amewaomba wote waliohudhuria kusimama kwa kutoa heshima ya kuwakumbuka maaskari 8 waliouwawa wakiwa katika ulinzi wa taifa. Itifaki katika hadhara hiyo ilizingatiwa

  • Rais Magufuli amewashukuru na kuupongeza uongozi wa chuo kikuu kwa kutoa sehemu ya kujengewa mabweni hayo, kaishukuru Wizara ya Elimu, kalishukuru na kulipongeza Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzania kwa kushirikiana na shirika la TBA katika kujenga na kusimamia ujenzi wa mabweni hayo. Katoa wito kwa Watanzania kuthamini ufundi na ustadi wa Watanzania wenzao kwa kutolea mfano wa shirika la TBA kwa kuonesha uzalendo wao kwenye ujenzi wa mabweni hayo

  • Kwenda mbali zaidi, Mheshimiwa Magufuli kaamuru wanafunzi wote watakaotumia mabweni hayo kulipa shilingi 500 tu, badala ya shilingi 800 ambazo wanalipa sasa, ili pesa zingine waweze kufanyia mambo mengine kwa kujiendeleza na kwa matumizi mengine ya maisha yao ya kila siku. Kwa kufanya hivyo, Mheshimiwa Rais kawasihi wanafunzi wajitahidi kwenye masomo na vilevile wayatunze hayo mabweni. Akasisitiza, awamu ya tano imedhamiria kuwekeza kwenye elimu kwa wanafunzi wote waliofikia vigezo kupata elimu bora

  • Akatoa ombi kwa vyombo vyote husika vya elimu kuwapa fursa wanafunzi kuchagua vyuo wanavyotaka badala ya kuchaguliwa, ili wapate elimu kwenye vyuo vyenye viwango vya juu na kwa matumizi bora ya pesa za serikali. Kahimiza wanafunzi wanaosomea udaktari kuhamishwa chuo kikuu kipya cha Muhimbili. Akaomba uongozi wa chuo kikuu kufufua mabasi ya chuo kikuu ili yaweze kuwasaidia na kuwapa wepesi wa usafiri wanafunzi na wahusika wa chuo kikuu

  • Mwisho katoa shukran kwa uongozi wa chuo kikuu, kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya chuo kikuu na shukran kwa waheshimiwa wabunge wote kwa kazi nzuri wanazozifanya na kwa kupitisha bajeti ya kujengwa kwa mabweni haya kwa pesa taslimu ya shilingi ya Tanzania

  • Kahimizi kuitanguliza Tanzania kwanza katika kuwaletea wananchi wa hali ya chini maisha bora na kawaomba waalimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi pamoja na kuwa na changamoto zinazowakabili

  • Kawaomba wananchi kuendelea kumpa ‘support’ kwenye kujenga taifa na akatoa shukran kwa waandishi wa habari na wasanii, na akamalizia kwa kusema “Mungu kibariki chuo kikuu cha Dar es Salaam”, Mungu wabariki wanachuo wote na waalimu, Mungu ibariki Tanzania…”

  • Baada ya uzinduzi wa mabweni hayo, Mheshimiwa Rais alielekea kuzindua majengo mapya ya Magomeni Kota ambayo pia ni moja ya ahadi yake aliyoiweka mwaka jana kwa wananchi wanyonge wa hali ya chini

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s