CCM YATOA KAULI YAKE JUU YA VITA VYA UKATILI WA MKOA WA PWANI NA VITA VYA KIUCHUMI

  • Baada ya kuona uzito wa jambo la usalama na amani nchini kwa wananchi, kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Mheshimiwa Pole Pole amekutana na waandishi wa habari kuelezea uzito wa matukio yanayoendelea maeneo ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti, Mkoa wa Pwani kuwa ni matukio yanayohusu usalama wa taifa na kwahivyo chama tawala chenye madaraka hakiwezi kuona haya matukio yakiendelea

  • Mheshimiwa Pole Pole amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikukaa kimya katika jambo hili bali kilikuwa kinafuatilia kwa ukaribu sana na hivyo wamebaini watu wenye matendo haya si watu wenye utu wala wenye hisia ya utu, na hakuna Mtanzania wa dini yoyote ndani ya nchi yetu, kwa umoja wetu, watakao unga mkono matendo haya ya kikatili ya kuwa na uwezo wa kuchukua roho ya mtu, isipokuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe

  • Amesisitiza, kwa kuelimisha umma, ama nje ya dini zetu, hakuna mtu yoyote ana mamlaka ya kuchukua roho ya mtu ila mamlaka ya nchi kisheria, pale tu mamlaka ya nchi inaposimamia haki za wananchi wake. Kwa matukio ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti, uongozi mzima wa CCM pamoja na wanachama wake wamesikitishwa sana na matukio hayo, na kama chama cha taifa, kitafuata sheria ya nchi na kitaendelea kufuatilia ukatili huu, amesema Mheshimiwa Pole Pole kwa hisia kubwa

  • Kwa niaba ya CCM, Mheshimiwa Pole Pole ametoa pole za dhati kwa wote walioguswa na matukio haya ya kidhalimu na amewaombea wote walioguswa moja kwa moja wapate faraja ya haraka ili warudi kwenye hali yao ya maisha ya kawaida ya kujenga taifa na chama bado kipo pamoja nao

  • Ameendelea kusema kwa msisitizo, watu wa Mkuranga, Rufiji na Kibiti ni Watanzania kweli kweli kama Watanzania wengine, na kwa hivyo, CCM itaiwajibisha serikali kuchukua hatua stahiki ili imani ya watu na hali ya amani irudi kwenye taifa letu lenye heshma kubwa duniani

  • Kutokana na wito huo, amezitaka rasilimali zote za vyombo vya ulinzi na usalama kutumika katika kuwaletea usalama na amani kwa wananchi wa Mkuranga, Rufiji na Kibiti badala ya hofu

  • Mheshimiwa Pole Pole amesikitishwa kuona baadhi ya watu wamekiachia chama tawala peke yake ndiyo kinachosimamia na matatizo ya wananchi kwasababu ya kulewa kwa madaraka na kujisahau kujenga mshikamano wa kitaifa, na kujisahau kujihusisha na maendeleo na shida za watu wetu mpaka wakati wa uchaguzi ufike. Amesisitiza kwa kutoa rai kwamba, Watanzania washikamane kwenye shida za wananchi bila ya kujali itikadi na amesikitishwa sana na hilo

  • Ameonya kuchezesha maneno wakati uhai wa wananchi upo hatarini. Akaongeza kwa kusema, ingawa ameshakutana na kufanya maongezi na baadhi ya viongozi wa kidini na wa kimila, lakini amesisitiza wasilikalie kimya tatizo hili (kwa moja kwa moja au kwa kuwakilishwa) na kwamba viongozi hawa wanaheshimika kitaifa na kisheria na hivyo viongozi wote wasimame pamoja

  • Mwisho amewaomba Watanzania kushikamana pamoja katika vita vya kujenga nchi kiuchumi, hususan amegusia maudhui yanayosemekana ya ulaghai yaliotokea kwenye makinikia ya madini ya taifa

  • Mheshimiwa Pole Pole amesema, anasikitishwa kuona kwenye jambo la maslahi ya taifa, kuna baadhi ya watu wanachagua upande wakati jambo hili ni la maslahi ya wazawa wa taifa hili na vizazi vyake, na huu ndiyo msingi wa CCM na ilani yake ya ujamaa na usawa. Alimalizia kwa kusema, kwenye jambo hili, Watanzania wote wasimame na Rais John Pombe Magufuli anayeitakia nchi yake ya Tanzania mema na mwenye kupenda umoja wa watu wake na taifa lake

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s