MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA VIWANDA NA BARABARA YA BAGAMOYO – MSATA, MKOA WA PWANI

 • Aupongeza Mkoa wa Pwani kwa maendeleo ya kilimo na viwanda

 • Awashukuru wananchi wa Pwani kwa kumpa kura wakati wa uchaguzi

 • Amshukuru Rais Mstaafu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake wa ujenzi wa barabara chini ya usimamizi wa wakati huo wa Mheshimiwa John Pombe Magufuli akiwa kama Waziri wa Ujenzi

 • Akemea ulaghai wa matumizi ya pembejeo hewa

 • Asisitiza halmashauri matumizi ya dawa za kuuwa vidudu vya maradhi ya malaria

 • Asisitiza kwa mwanafunzi wa kike anayepata mimba ni marufuku kurudi shuleni iwapo ataamua mwenyewe kufuata njia hiyo; na kwa anayetia mimba mwanafunzi sheria ifuate mkondo wake

 • Afafanua serikali inagharamia pesa nyingi kutoa elimu bure katika kuelimisha watoto wa taifa la kesho na kwahivyo mwanafunzi atakayeamua kuchukua mimba atakaa nyumbani

 • Ampongeza Mheshimiwa Mama Salma Kikwete kwa kulisimamia suala hilo bungeni

 • Aliendelea kukana vikali ushoga na matendo ya jinsia moja

 • Atuma ujumbe mkali kwa taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zenye kupandikiza tamaduni na maadili ambayo ni kinyume na maadili ya Tanzania

 • Aonesha makubwa kwa wakazi wanyonge kwa kuwasaidia na kuwarudishia ardhi yao wanapojipatia rizki zao na watoto wao

 • Asisitiza wananchi waendelee kumuombea Mungu

 • Mwisho, wakati akiwa tayari kuzindua barabara ya Bagamoyo – Msata, agusia wanaotoa ardhi kwa wawekezaji huku wakiwanyanyasa wananchi wanyonge

 • Awashukuru wakazi wa Mkoa wa Pwani na alishukuru Jeshi la Magereza

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU, MKOA WA PWANI

 • Atembelea viwanda mbalimbali Mkoa wa Pwani, vikiwemo viwanda vya matrekta na vifungashio

 • Aushukuru uongozi wa India kwa msaada wao kwenye miradi ya maji

 • Awapongeza wakuu wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kwa kulinda miundombinu ya maji

 • Awapongeza wahusika wa miradi ya maji kwa kazi wanazozifanya

 • Aiagiza Dawasco wamalize miradi yote iliyokuwa haijaisha ukiwemo mradi wa Lindi

 • Asisitiza kulipwa kwa kodi ya maji kwa wakati

 • Ausifia mradi wa maji wa Ruvu Juu ulivyokamilika kwa ujenzi wa hali ya juu

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA MKOA WA PWANI KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TATU KWENYE UZINDUZI WA VIWANDA NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 • Asisitiza mshikamano miongoni mwa Watanzania katika kujenga Tanzania ya viwanda

 • Aupongeza uongozi wa Mkoa wa Pwani

 • Aonya wanaonyanyasa wananchi wanyonge wa hali ya chini

 • Aagiza viongozi wote kulinda maslahi ya wananchi wanyonge na maslahi ya wananchi wa hali ya chini

 • Aonya wahalifu wachache wa Kibiti na Rufiji

 • Ahimiza viwanda vya ndani kwa manufaa ya Watanzania wote

 • Aagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhimiza wananchi kufanya kazi

 • Awaomba wananchi waendelee kumuombea Mungu na wamuamini katika kuisaidia nchi na wananchi wa Tanzania kwa ujumla