MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA VIWANDA NA BARABARA YA BAGAMOYO – MSATA, MKOA WA PWANI

 • Aupongeza Mkoa wa Pwani kwa maendeleo ya kilimo na viwanda

 • Awashukuru wananchi wa Pwani kwa kumpa kura wakati wa uchaguzi

 • Amshukuru Rais Mstaafu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake wa ujenzi wa barabara chini ya usimamizi wa wakati huo wa Mheshimiwa John Pombe Magufuli akiwa kama Waziri wa Ujenzi

 • Akemea ulaghai wa matumizi ya pembejeo hewa

 • Asisitiza halmashauri matumizi ya dawa za kuuwa vidudu vya maradhi ya malaria

 • Asisitiza kwa mwanafunzi wa kike anayepata mimba ni marufuku kurudi shuleni iwapo ataamua mwenyewe kufuata njia hiyo; na kwa anayetia mimba mwanafunzi sheria ifuate mkondo wake

 • Afafanua serikali inagharamia pesa nyingi kutoa elimu bure katika kuelimisha watoto wa taifa la kesho na kwahivyo mwanafunzi atakayeamua kuchukua mimba atakaa nyumbani

 • Ampongeza Mheshimiwa Mama Salma Kikwete kwa kulisimamia suala hilo bungeni

 • Aliendelea kukana vikali ushoga na matendo ya jinsia moja

 • Atuma ujumbe mkali kwa taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zenye kupandikiza tamaduni na maadili ambayo ni kinyume na maadili ya Tanzania

 • Aonesha makubwa kwa wakazi wanyonge kwa kuwasaidia na kuwarudishia ardhi yao wanapojipatia rizki zao na watoto wao

 • Asisitiza wananchi waendelee kumuombea Mungu

 • Mwisho, wakati akiwa tayari kuzindua barabara ya Bagamoyo – Msata, agusia wanaotoa ardhi kwa wawekezaji huku wakiwanyanyasa wananchi wanyonge

 • Awashukuru wakazi wa Mkoa wa Pwani na alishukuru Jeshi la Magereza

Advertisements