MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 422 WA JWTZ KATIKA SHEREHE ZILIZOFANYIKA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID, JIJINI ARUSHA

 • Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli atunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 wa Jeshi la Wananchi Tanzania kwenye sherehe iliyofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha

 • Katika sherehe hizo, Mheshimiwa rais awapongeza makamanda waliotoa mafunzo ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi na alipongeza jeshi la Tanzania kwa kulinda amani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

 • Alihakikishia jeshi la ulinzi kuwa jeshi la kisasa na akatangaza neema ya ajira elfu tatu kwa wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania

 • Shangwe na vifijo vya wananchi vilirindima baada ya ndege za kivita ziliponguruma kwenye anga za mipaka ya Tanzania wakati Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Arusha

 • Mheshimiwa rais akaelezea umma wa Tanzania, hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya tano ya kudhibiti ufisadi na rushwa, hatua ambazo ndiyo zimeleta maendeleo makubwa tangu aingie madarakani, kwa mfano ununuzi wa ndege mpya za taifa, reli ya kisasa ya mwendo kasi, elimu bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi mpaka sekondari, usambazaji wa maji mijini na vijijini, mradi mkubwa uliokuwa ndoto ya baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge uliopo Rufiji, na maendeleo mengineyo mengi ambayo ameyafanya kwa kipindi cha muda mfupi sana tangu aingie madarakani

 • Atoa wito kwa Watanzania popote pale walipo waweke Utaifa Kwanza kabla ya kitu chochote kwa mafanikio ya Watanzania wote; na asihi kwa kufanya hivyo, Watanzania wote kwa umoja wao watanufaika

 • Aelezea jinsi alivyojitolea kulitumikia taifa kwa manufaa ya Watanzania wote na anachokiomba kwa Watanzania wote ni kuendelea kumuunga mkono bila ya kujali itikadi zao za kivyama/kisiasa au itikadi za kidini

 • Asisitiza kwa mara nyingine tena, viongozi wote wa ngazi zote za mikoa na wengineo kushughulika na kutatua kero za wananchi kwenye maeneo yao na kuwaletea maendeleo

 • Aelezea kuiva kwa mipango ya harakati za makao makuu ya taifa kuhamia Dodoma na awaomba viongozi wote kujipanga kuhamia Dodoma

 • Aelezea hatua zilizochukuliwa na serikali za kuondosha tozo kwa wakulima ili wakulima wapate kunufaika na mazao yao na kukuza hali yao ya kiuchumi

 • Alihakikishia jeshi kuwa analipenda na atashughulikia changamoto zao

 • Aagiza mabango yote yaliyofika kwenye hadhara hiyo yasomwe hadharani kupata uhalisia wa kero za wananchi na ameagiza kero hizo zishughulikiwe na ngazi zote za mkoa

 • Mwisho, wanachama wa vyama vya upinzani walijitokeza hadharani kurejea kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa kuona mheshimiwa rais anazisimamia sera za CCM kisawasawa. Mheshimiwa Rais alihitimisha kwa kuliombea taifa na watu wake