MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AMTEUA MHESHIMIWA MOHAMMED ALI AHMED KUWA NAIBU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ZANZIBAR

Kutoka Ikulu.

Advertisements

BARAZA LA EID, KWA NIABA YA MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI, MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA AWASIHI WATANZANIA KUENDELEA KUTENDA MATENDO MEMA

* Ni baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

RAIS Dkt. John Magufuli amewaasa Waislam na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kutenda mema baada ya kuwa wamejisahihisha na kutubu makosa yao ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 
Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Juni 15, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli kwenye Baraza la Eid El Fitr lililofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Mkuu amesema Viongozi wanaendelea kuwasihi Waislam wote na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuonesha upendo, umoja na kuvumiliana  hasa baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 
Amesema huruma, ukarimu na ucha Mungu ulioneshwa katika kipindi cha mfungo wa ramadhani, uendelee na uwe sehemu ya maisha ya kila siku na kamwe usiwe umeisha baada ya mwandamo wa mwezi wa mfungo mosi.
 
Waziri Mkuu ameongeza kuwa upendo, umoja, utulivu, mshikamano na subra uliooneshwa kipindi chote cha mfungo wa ramadhani ni vema ukaendelezwa kwa sababu ucha Mungu si katika mwezi huo pekee.
 
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameniagiza kwa kusema ‘’Waislam ni kielelezo cha taasisi za dini zinazozingatia maadili mema, hivyo wachache wasijipenyeze na kuharibu taswira yao. Ninawahakikishia kuwa Serikali iko tayari kushirikiana taasisi yeyote ya dini ambayo itakuwa tayari kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na taratibu tulizojiwekea nchini’’
 
Amesema wakati huu wa kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vema wakakumbuka maneno ya Mtume Muhammad (S.A.W) kwamba ‘’Mwenye kufanya maasi siku ya Eid ni sawa na kumuasi Allah Sub-hanahu Wata’ala siku ya kiyama,’’.
 
Hivyo amewaasa wananchi wanaposherehekea siku kuu ya Eid El Fitr waendelee kudumisha amani na utulivu kwa kujiepusha na vitendo vibaya vinavyoashiria vurugu, uonevu na uvunjifu wa amani kwa kuwa havina tija.
 
Awali, Sheikh Mkuu na Mufti waTanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally alitoa wito kwa Masheikh wa Mikoa na Wilaya zote nchini wahakikishe kila wanapofanya mikutano yao mada ya amani na kudumisha uzalendo zisikose kwa kuwa ni vitu muhimu.
 
‘’Kama mtu huna uzalendo hata dini inapungua, tujenge uzalendo kwa ajili ya kuienzi nchi na kuifanya iendelee kuwa kisiwa cha utulivu. Tuendelee kujenga umoja na mshikamano tusiliache suala hili kwa sababu ndilo liloijenga jamii yetu,’’ alisema.
 
Pia Mufti Zubeir alisema ni vizuri kwa waislam waunge mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na waache kuishi kwa mazoea. ’’Rais wetu Dkt. Magufuli anafanya kazi kubwa hivyo ni lazima tumuunge mkono na kumpongeza.’’
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir  (wapili kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salim (wapili kushoto) baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika  Baraza la Eid, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) kuingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Baraza la Eid Juni 15, 2018. Wapili kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salim.
Baadhi ya waliohudhuria katika Baraza la Eid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo akimwakilisha  Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 15, 2018.

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiteta na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir katika Baraza la Eid kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoj jijini Dar es salaam Juni 15, 2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli . 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 15, 2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Source: Michuzi blog

SWALA YA EID-EL-FITR MKOANI TABORA, WAISLAM MKOANI TABORA WAMPONGEZA MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KWA MISAADA YAKE

SHEIKH wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amemupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kusaidia shughuli mbalimbali za kuendeleza miradi ya madhehebu mbalimbali ikiwemo  ya Waislamu hapa nchini.

Alitoa kauli hiyo mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora

Sheikh Mavumbi alisema misaada anayochangia ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za Ibada ni jambo zuri na linamuonyesha kuwa yeye sio mbaguzi  na ameonyesha mapenzi makubwa aliyonayo kwa watu wote bila kujali tofauti zao , hali inayosaidia kuimarisha umoja wa Kitaifa ulioasisiwa tangu uhuru wa Nchi ya Tanzania.

Sheikh huyo wa Mkoa aliwataka Waislamu wote nchini kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli na Serikali yake katika jitihada zake mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo hapa nchini.

Alitoa wito kwa wakazi wote Mkoani hapa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kudumisha mshikamano na upendo ili amani iliyopo iendelee kudumu na waumini waendelea kusali bila wasiwasi katika nyumba zao za Ibada.

Aidha Sheikh Mavumbi aliwataka Masheikh wa ngazi zote na Maimam kuhakikisha kuwa ndoa wanazofungisha zingatie maandiko matakatifu ili kuepuka kusababisha kuwepo na ndoa za utotoni mkoani humo.

Alisema ni vema kabla ya kufungisha ndoa  viongozi hao wakahoji ili kujua kama binti anayekusudiwa kufungishwa ndoa umri wake unaostahili na sio mtoto.

Kwa upande wa suala la elimu Sheikh huyo aliwasisitiza Waislamu wote kuhakikisha wanawahimiza watoto kuzingatia masomo na kuhudhuria shuleni bila kukosa ili kuuepusha Mkoa wa Tabora kuwa miongoni mwa Mikoa inaoongoza kwa watoto watoro.

Alisema hata Mtume Muhammad SAW pamoja na kutoa mafunzo elimu ya dini anawahimiza Waislam watafuete elimu hata ikiwa mbali kama vile China na kuongeza ndio maana ni vema kuwahimiza watoto wasome.

Akitoa salamu za Eid El Fitri kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza aliwataka Waislamu wote kuonyesha wamefuzu kwa kuendeleza mema yote waliofundishwa na viongozi wa dini kwa ajili ya kudumisha amani na upendo hapa nchini.

Alisema mafundisho waliyopata katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yakawe Darasa la kuwafanya Waislam waendelee kutii Sheria za Nchi na Serikali kwa ajili kuendelea kuwa na mazingira mazuri na tulivu ya kufanya Ibada.

Naye Sheikh wa Wilaya ya Tabora Ramadhan Rashid aliwataka Waislam Mkoani Tabora kutumia mafunzo waliyoyapata katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuendeleza mazuri yote na kuacha vitendo kama vile ulevi, ugomvi, uzinifu na vingine ambavyo vitawafanya kutenda dhambi.

Alisema ni vema kuanzia sasa na kuendelea wakaendeleza mshikamano , upendo na matendo ya uhuru kwa ajili ya kudumisha amani na utulivu baina yao na watu wa madhehebu mengine.

 

1

Sheikh  wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi (mbele) akiongoza Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

2

Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislaam wakiwa katika Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

3

Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislaam wakiwasili kwa ajili ya kushiriki Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora

4

Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislaam wakiwali Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

5

Sheikh  wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi (mbele) akisikiliza salamu za Eid El Fitri kwa niaba ya Serikali kutoka kwa  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

6

Baadhi wakimama wa dini ya Kiislam wakisikiliza salamu za Eid El Fitri kwa niaba ya Serikali kutoka kwa  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza (hayupo katika picha) mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

7

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza akitoa salamu za Serikali mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

8

Baadhi ya Wakinababa wa dini ya Kiislam wakisikiliza salamu za Eid El Fitri kwa niaba ya Serikali kutoka kwa  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza (hayupo katika picha) mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

Source: Michuzi blog

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHESHIMIWA ALI MOHAMMED SHEIN AHUTUBIA BARAZA LA EID ZANZIBAR

 

 Msafara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ukiwasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar,Rais akihudhuria katika Baraza la IDD-EL-FITRI lililofanyika leo katika kusheherekea Sikukuu ya Eid baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Katiba,Sheria.Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, leo akihudhuria katika Baraza la  IDD-EL-FITRIlililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Eid baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  na Waziri wa Katiba,Sheria.Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (katikati) wakifuatana mara alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, leo akihudhuria katika Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya IDD baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud na Kamishana wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (mbele) akipokea salamu ya Heshma ya Gwaride la Kikosi cha Polisi FFU leo mara alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, katika Baraza la  IDD-EL-FITRI   lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Eid baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Askari wa Kikosi cha Polisi (FFU) wakitoa salamu ya Heshma kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, katika Baraza la  IDD-EL-FITRI  lililofanyika leo  katika kusheherekea Sikukuu ya Eid baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Waziri wa Katiba,Sheria.Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (kulia)  mara alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, leo akihudhuria katika Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Idd baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan (kushoto) Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassan Haji
 Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakiwa katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar katika Sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Idd baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan  lililofanyika leo Mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 Waziri wa Katiba,Sheria.Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (katikati) alipokuwa akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), ili kuzungumza na Wananchi na Viongozi katika Baraza la  IDD-EL-FITRI  ikiwa ni katka kusherehekea  Sikukuu ya Eid baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hafla iliyofanyika leo  katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiwahutubia viongozi,Mabalozi,Wananchi na Waislamu mbali mbali katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
 Baadhi ya Viongozi wakisikiliza na kuangalia Vitabu vya Hutuba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) aliyoitoa leo katika Baraza la  IDD-EL-FITRI ikiwa ni kusherehekea Sikukuu baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan sherehe zilizofanyika katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
 Baadhi ya Viongozi Wanawake na Wanaume wakiangalia vitabu na kumsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo  katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,zilizofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiwahutubia Viongozi,Mabalozi,Wananchi na Waislamu mbali mbali katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiwahutubia viongozi,Mabalozi,Wananchi na Waislamu mbali mbali katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
 Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wakiangalia vitabu na kumsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo  katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,zilizofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
 Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakiwa katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar katika Sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Idd baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan  lililofanyika leo Mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein 
 Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Gharib Bilal,Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Amani Abeid Karume na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) wakichukua chakula baada ya sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  lililofanyika leo katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na wananchi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika leo katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na IKULU. 
Source: Michuzi blog

SWALA YA EID MSIKITI WA ANWAR, MSASANI, JIJINI DAR ES SALAAM

a1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika  sala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni 15, 2018.

a2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika sala ya Eid kwenye Msikiti  Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

a3

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Waislamu baada ya kushiriki katika sala ya Eid  kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

a4

Waziri   Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kushiriki katika sala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Source: Michuzi blog