KESHO KIPINDI MAALUM CHA MAENDELEO YA TRENI MPYA YA KISASA (SGR) KUANZIA SAA 1 USIKU TBC1

Advertisements

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHI HATI ZA VIWANJA VYA DODOMA KWA WAWAKILISHI WA KIMATAIFA

 • Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli akabidhi hati za viwanja vya Dodoma kwa wawakilishi¬† wa kimataifa ikiwa moja ya harakati za kuhamia jiji la Dodoma ambalo pia ni Makao Makuu ya Tanzania

 • Katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais atambua uwepo wa viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi na awashukuru kwa kuhudhuria katika hafla hii ya kihistoria ya harakati za kuhamia Dodoma tangu itangazwe mwaka 1973 na kutimiza azma na ndoto ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

 • Aainisha kwamba mpaka sasa viongozi wa serikali wameshahamia Dodoma akiwemo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, na kabla ya mwisho wa mwaka huu Mheshimiwa Rais anatarajia kuhamia Dodoma, alisema Mheshimiwa Rais Magufuli

 • Awapongeza viongozi wa Dodoma kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kutekeleza matayarisho ya uhamiaji wa Dodoma, na aelezea utoaji wa hati na viwanja bila ya malipo ni mfano wa ushirikiano wa Tanzania

 • Aelezea harakati mbalimbali zinazofanyika jijini Dodoma za kuendeleza miundombinu ya barabara, miundombinu ya umeme, huduma za afya, maji, huduma za jamii, na huduma za elimu

 • Pamoja na jitihada mbalimbali za miundombinu, pia Mheshimiwa Rais ameshatoa maagizo kuanzwa kwa kutangazwa kwa zabuni ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato, Dodoma, ili ndege za Air Tanzania na ndege za kimataifa ziweze kutua na kurahisisha usafiri wa jiji la Dodoma

 • Aelezea matarajio ya ndege mbili za Bombardier CS300 ambazo zinatarajiwa kuwasili mwezi Novemba mwaka huu, na ndege nyingine ya Boeing 787-8 Dreamliner kuwasili mwishoni mwa mwaka ujao

 • Aainisha kwamba nchi nzima kuna manispaa 21, kuna halmashauri za miji 22, kuna halmashauri za wilaya 137, na kuna miji 6 yenye sifa za majiji. Lakini katika sehemu zote hizo, jiji la Dodoma ndiyo inaongoza kwa ukusanyaji wa mapato

 • Atoa mfano Dodoma imekusanya bilioni 24.2 badala ya bilioni 19 iliyojipangia, Dar es Salaam imekusanya bilioni 15.3 badala ya bilioni 16.4 iliyojipangia, Arusha imekusanya bilioni 10.3 badala ya bilioni 13.9 iliyojipangia, Mwanza imekusanya bilioni 9.3 badala ya bilioni 12.5 iliyojipangia, Tanga imekusanya bilioni 9.1 badala ya bilioni 18.3 iliyojipangia, Mbeya imekusanya bilioni 4.2 badala ya bilioni 9.6 iliyojipangia

 • Kutokana na matokeo hayo, Mheshimiwa Rais Magufuli awahamasisha mabalozi kuhamia Dodoma kwa kuonesha jinsi Dodoma inavyopiga hatua

 • Ampongeza Mkurugenzi wa Dodoma, Mheshimiwa Godwin Kunambi kwa kazi nzuri anyoifanya, na pia aupongeza uongozi wa jiji la Dodoma

 • Kwenye manispaa, Mheshimiwa Rais Magufuli aainisha manispaa ya Shinyanga ndiyo inayoongoza, na manispaa ya mwisho ni manispaa ya Kinondoni ambayo imekusanya asilimia 22

 • Kwenye halmashauri za miji, Geita imekusanya bilioni 7.4 zaidi badala ya bilioni 3.2 ilivyojipangia, na halmashauri ya miji ya mwisho ni halmashauri ya Mbulu ambayo imekusanya asilimia 34

 • Kwenye halmashauri za wilaya, Kibaha ndiyo inayoongoza, na halmashauri ya wilaya ya mwisho ni halmashauri ya Mbinga

 • Takwimu hizi Mheshimiwa Rais Magufuli aonesha kwamba Dodoma ni jiji linalokuwa na awahamasisha kuhamia haraka lakini kwa utaratibu na mpango waliojiwekea wao, na awahakikishia kuwapa ushirikiano

 • Awaelezea jinsi Tanzania mpya inavyopambana na rushwa, wafanyakazi wenye veti bandia, wafanyakazi hewa, kubana ufisadi, kukua kwa mapato ya kodi kutoka bilioni 850 mpaka kufikia trilioni 1.3 kwa mwezi ndani ya miaka miwili na nusu, kuongezeka kwa nidhamu ya wafanyakazi maofisini, utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, kuongezeka kwa madawa, miradi ya umeme ya Kinyerezi na Steigler’s Gorge ambayo itachochea kwenye uchumi wa viwanda na kurudisha gharama za umeme chini kwa matumizi ya ndani ya nchi

 • Aelezea ubadhirifu wa madini na hatua zilizochukuliwa na serikali kudhibiti madini hayo kwa maslahi ya taifa kwanza, na vilvile aelezea udhibiti wa mfumko wa bei

 • Mwisho awashukuru wote waliohudhuria kwenye hafla hiyo na awakaribisha kwenye dhifa ya chakula, na awaombea baraka pamoja na Watanzania