MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

ccm1

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na wajumbe wengine wakiwa wamesimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka na kuwaombea majeruhi na waliopoteza maisha katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 katika ziwa Victoria kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba, Jijini Dar es Salaam, Septemba 29,2018.

ccm2

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba, Jijini Dar es Salaam, Septemba 29, 2018.

ccm3

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt. John Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mweyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba, Jijini Dar es Salaam, Septemba 29, 2018.

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA AMIRI WILLIAM ARTHUR PHILIP LOUIS WA PILI KWENYE MSTARI WA UFALME WA MALKIA ELIZABETH II, JIJINI DAR ES SALAAM, IKULU

magufuli

Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli pichani akimkabidhi Amiri William Arthur Philip (Prince William), picha ya wanyama pori wakali watano (The big five) wanaopatikana katika mbuga za wanyama mbalimbali nchini Tanzania. Pichani wakishuhudia tukio hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Khamis Kigwangalla, na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Palamagamba Kabudi.

magufuli1

Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli apokea picha kutoka kwa Amiri William Arthur Philip (Prince William), picha inayo muonesha baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa anazungumza na Malkia wa Uingereza, Elizabeth II.