Mfuko Wa Maziko UK

100220111121

Alhamdulillah, jana hapa mjini London nimepokea utambulisho wangu kutoka jumuiya ya Tawhiyd inayoshughulikia Mfuko wa Maziko UK ambayo makao makuu yake yapo Northampton, UK.

Malipo yake ni ya wepesi kabisa kwa njia ya intaneti ‘online transfer’ ambayo mimi binafsi nimetumia (kwa malipo ya £60 kwa mwaka mzima), au vilevile unaweza kutumia njia ya kulipa £5 kila mwezi, au kwa njia ya kuweka benki (deposit).

Tuombe Allah atupe uzima wa afya; kwa wingi tutakavyojiunga na mfuko huu, ndio mfuko huu utapata nguvu na isitoshe utatufaa wenyewe katika mambo ya maziko na utawafaa watoto wetu kwenye mambo ya maziko inshallah.

Kwani bila ya kujiunga na chombo kama hiki popote pale ulipo hasa huku ugenini, au bila ya kuwa na chombo kama hiki katika jamii ni mara nyingi huwa tunawapa uzito jamii na uzito familia zetu.

Mfuko huu wa maziko umeanzishwa na unaongozwa na kamati ya jumuia ya Waislam Waswahili wa kutoka Tanzania waliopo UK (Tawhiyd).

Tunataraji kila mwenye nia kwenye jamii ya kujiunga na mfuko huu basi usisite, kwani kila mtu litamfika jambo la mauti aidha kwake au kwa mtu wake wa karibu, inshallah. Kwa maelezo zaidi bonyeza kwenye link ifuatayo: http://www.tawhiyd.com

Kama kuna hoja yoyote, ni wajibu wa kila mtu katika jamii kufuatilia jambo kwa binafsi yako aidha kwa kupigia simu wahusika au kutuma barua ili upate undani wake kuliko kungoja kusikia kwa watu maneno tofauti na mwisho ikampeleka mtu kwenye ‘dhanna’ ambayo humpeleka mtu kwenye ‘dhambi’.

Vilevile kama ilivyoandikwa hapo siku za nyuma kwa ndugu, rafiki na jamaa ambao wapo nje ya UK au nje ya Tanzania wawe wa dini yoyote ile, kama watapendelea rai ya kuanzisha mfuko kama huu kwa kuunda kamati maalum husika ili kuwe na wepesi wa kutayarisha maziko mara tu msiba unapotokea kwa mwenzetu ili mwili ukapumzishwe baada ya kutangulia mbele ya haki.

Date posted: February 11, 2011

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s