Ajali Inayongoja Kutokea

shimo

Shimo moja wapo la kutatulia matatizo ya miundo mbinu ya maeneo ya Kariakoo lipo matatizoni na muda si mrefu sana litasababisha ajali kubwa kwa wapita njia hii.Shimo hili ambalo lipo mtaa wa Sikukuu baina ya mtaa wa Ndovu na Twiga limefikia hali ya kuwa wakati wowote kuanzia sasa mfuniko wa shimo hilo litazama na mtu iwapo mfuniko huo utakanyagwa na mtu ambaye hajaliona shimo hilo na kuelekea kusababisha ajali kubwa kwa mtu huyo.

Maeneo haya ya mtaa wa Sikukuu hupitwa na mamia kama si maelfu ya watu na magari kila siku tena kwa kishindo, shimo hili limekaa katika hali hii kwa muda mrefu sasa na inasemekana na imethibitika kuwa diwani wa maeneo haya ameshapeleka maelezo kuhusu hali ya shimo hili kwa wahandisi wahusika kwa kupitia mwenyekiti wa serikali za mitaa lakini mpaka hivi sasa hakuna dalili yoyote wala upelelezi wa mwanzo wa hali ya shimo hilo kufanyika na wahandisi wahusika.

Mashimo haya yanapofikia hali hii na yapatapo vishindo vya magari hufanya mtikisiko wa ardhi na hupelekea hata kuta za nyumba zilizopo mkabala na mashimo hayo kutikisika kutokana na vishindo hivyo, kwahiyo ni muhimu mashimo haya kupitiwa na wahandisi na mara baada yanapoanza kuharibika au kabla hata ya kufikia hali kama iliyopo hapo juu pichani kufanyiwa ukarabati wa haraka kuepusha ajali zinazongojea kutokea kutokana na hali ya mfuniko wa shimo uliopo pichani juu.

Jumapili ya wikiendi iliyopita, inasemekana kulikuwa kuna mama mmoja alikwenda kwenye harusi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Hall kwenye majira ya saa mbili na nusu au saa tatu usiku, mama huyo alishuka kwenye gari aliyopelekwa na mtoto wake nje ya ukumbi huo na hapo hapo nje kulikuwa na shimo ambalo halina mfuniko (manhole cover) na kusababisha mama huyo kuingia mzima mzima kwenye shimo hilo na kujeruhika vibaya sana katika mwili wake. Kilichomsaidia mama huyo, aliwahi kukinga na kupanua mikono yake miwili ikamwezesha asiingie mwili mzima  kwenye shimo hilo.

Kwa niaba ya usalama wa watumia njia na wapita njia na mazingira kwa ujumla, naomba wahandisi wahusika wa maeneo haya na mengine jijini waliangalie tena tatizo la mashimo haya hususan shimo hili linalo omba msaada, kwa kelele kubwa isiyosikika.

Samahani kama nimekosea.

Ndugu yenu,

Saleh Jaber

Date posted: April 11, 2013
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s