Fainali Za Mashindano Ya Kuhifadhi Qur’an Afrika Mashariki Na Kati

7_2

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo na kushirikisha jumla ya wshiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.


5_1

Mshiriki kutoka Tanzania, Ibrahim Ramadhan, akishiriki fainali za mashindano hayo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.


6_1

Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an, ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano hayo,Mohammad Sad Tawfiq, kutoka Egypt akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi wa fainali hizo zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

 

4_2

Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an, ambaye alishika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo,Jahuddin Adam, kutoka Sudan akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi wa fainali hizo zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

 

3_2

Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an, ambaye alishika nafasi ya pili katika mashindano hayo, Kombo Bahi Makame kutoka Unguja-Tanzania, akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi katika fainali hizo zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

 

8_1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an, Jahuddin Adam, kutoka Sudan,baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo, zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 

1_1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, kuhudhulia Fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu iliyofanyika kwenye ukumbi huo na kuwashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.

 

2_1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo wakifuatilia kwa makini fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an.

 

10_1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an, zilizofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamondi Jubilee jijini Dar es Salaam, na kuwashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.

 

11

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an, baada ya kutangazwa washindi katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo.

 

12

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Mashindano Ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu Yafana Jijini Dar es Salaam Leo

Dsc_8369

Sehemu ya Mashekhe na umati wa Waislamu uliofurika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar es salaam kushuhudia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu yaliyoshirikisha wanafunzi wa madrasa toka Bara na visiwani

Dsc_8373

Sehemu ya washindani wavulana


Dsc_8456

Washindani wasichana


Dsc_8503

Mke wa rais Salma Kikwete (wa pili kulia) akimsaidia kuwasha Pikipiki ya kubeba mizigo Mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Qur’an juzu 30 Khalid Omar Mbarouk (15) katikati wa Madrasat An-Nujum ya Temeke yaliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Jaji wa Hifadhi, Hassan Ahamed Katunguya na kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano ya kuhifadhi Qur’an nchini Bi Aisha Sururu.

 

Img_4222

Mke wa Rais Salma Kikwete (watatu kulia) akimkabidhi funguo za pikipiki ya kubebea mizigo aina ya Bajaj iliyotolewa na Home Shopping centre kwa Mshindi wa kuhifadhi Qur’an juzu 30 Khalid Omar Mbarouk (kulia) wa Temeke Dar es salaam baada ya kuibuka mshindi katika Mashindano ya kusoma kwa kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

Img_4201

Mke wa Rais Salma Kikwete (watatu kulia) akiwa mwanaharakati maarufu na mratibu wa shindano hilo Bi Aisha Sururu wakiomba dua baada ya shindano hilo lililofana sana

Source: Michuzi Blog

Tatizo La Mafuta Jijini Laanza Kupungua

10082011302

Baada ya serikali kutamka bungeni juzi kuwa vituo vyote vya mafuta vinalazimika kuanza kutoa mafuta baada ya mgomo wa siku kadhaa, baadhi ya vituo vikionekana kuanza kutoa huduma hiyo ya kuuza mafuta na baadhi ya vituo bado vikikaidi amri ya serikali ambayo ilitoa masaa 24 kuitikwa kwa mwito huo.

Wabunge mbalimbali walihojiwa mchana jana kwenye vyombo mbalimbali vya habari, walisisitiza umuhimu wa amri hiyo ambayo serikali ilitoa kwa wauzaji mafuta siyo kwasababu ya kuwaadhibisha kutokana na makadirio ya serikali bali mafuta ndio uti wa mgongo (backbone) wa uchumi wa taifa na ni muhimu mafuta yapatikane katika kuendesha uchumi na maendeleo mengine ya kijamii (social mobility).

Kwa muda gani mafuta hayo yataendelea kupatikana, hilo ni suala la wasaa.

Ramadhan 2011

A Nepalese Muslim reads the Qur'an in a day of the month-long fasting during the holy month of Ramadhan in Kathmandu.