Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan mjini Unguja.
Rais Dkt. Ali Mohamed Shein, pichani juu, akionekana akila kiapo cha kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa miaka mitano ijayo, kwa matarajio ya dira ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar sambamba na dira ya taifa ya mwaka 2025. [Picha na Ikulu.]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Mungu ibariki Tanzania, Viongozi wake na Watu wake. Amin.