MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA BURUNDI MHESHIMIWA ÉVARISTE NDAYISHIMIYE KATIKA ZIARA YA KIKAZI, WAKUBALIANA KUKUZA MIRADI YA KIUCHUMI NA KIMAENDELEO BAINA YA NCHI MBILI, RAIS MAGUFULI AIPONGEZA BURUNDI KWA KUENDELEZA AMANI NA UTULIVU NCHINI, AMPONGEZA RAIS NDAYISHIMIYE KWA KUONGEA KISWAHILI FASAHA, MHESHIMIWA RAIS NDAYISHIMIYE AMPONGEZA MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI KWA MAENDELEO YA KASI ALIYOLETA NCHINI TANZANIA KWA MUDA MFUPI, ASEMA WANA BURUNDI WANGEMPA KURA ZOTE ZA KUENDELEA KUWA RAIS, AMTAKIA MAFANIKIO YA KUPATA KURA NYINGI ZA KUIONGOZA TANZANIA KWA MIAKA IJAYO

MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA AUNGANA NA VIONGOZI MBALIMBALI AKIMUWAKILISHA MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUUAGA NA KUUPUMZISHA MWILI WA JAJI MKUU MSTAAFU MARK BOMANI JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi  wakati alipowaongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa Mwanasheria  Mkuu Mstaafu, Mark Bomani kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mwanasheria Mkuu  Mstaafu, Mark Bomani kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 14, 2020. Wengine pichani kutoka kushoto ni Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, Waziri Mkuu Mstaafu Josph Warioba, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipowaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mwanasheri Mkuu Mstaafu, Mark Bomani kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Bomani kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya wakati alipowaongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa Mwanasheria  Mkuu Mstaafu, Mark Bomani kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)