MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI KUPIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI CHAMWINO JIJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan apiga kura kuchagua Viongozi wa Shina namba 1, Tawi la Chamwino, Wilayani Chamwino, Dodoma. (Picha na Adam H. Mzee).

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo (kushoto) na Katibu wa NEC Ndugu Moudline Cyrus Castico (kulia). (Picha na Adam H. Mzee).

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kupiga kura na kuchagua Viongozi wa Shina namba 1, Tawi la Chamwino, Wilayani Chamwino, Dodoma. (Picha na Adam H. Mzee).

MHESHIMIWA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ATOA PONGEZI LA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

MHESHIMIWA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKIWA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHESHIMIWA MWIGULU LAMECK NCHEMBA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI WASHINGTON DC NCHINI MAREKANI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makao Makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), jijini Washington DC, Marekani, wakati Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bi. Kristalina Georgieva.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Kanda ya Afrika Bw. Abebe Selassie, jijini Washington DC, Marekani.

Ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), ukiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya IMF, jijini Washington DC, Marekani. Wanaofuatia ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bi. Sauda Msemo, Mshauri mwandamizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika, Dkt. Zarau Kibwe na Katibu Mkuu Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil.

Ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto), ukiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya IMF, jijini Washington DC, Marekani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango, Washington DC)

SHEREHE ZA KUMBUKIZI YA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWA MWALIMU NYERERE ILIYOJUMUISHA FAMILIA YA MWALIMU AKIWEMO MAMA MARIA NYERERE NA MAKONGORO NYERERE NA VIONGOZI NA WADAU MBALIMBALI WAALIKWA AKIWEMO RAIS WA ZANZIBAR AKIMUWAKILISHA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA MAMA SAMIA SULUHU HASSAN, MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA, WAZIRI MKUU, NAIBU SPIKA WA BUNGE, OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA, NA VIONGOZI WASTAAFU, VIONGOZI WOTE WAMEELEZEA KAZI KUBWA ILIYOFANYWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE YA UJENZI WA TAIFA LA TANZANIA

MHESHIMIWA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA CHEMBA YA BIASHARA MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Marekani, Suzanne Clark, mara baada ya mazungumzo katika ofisi za chemba hiyo jijini Washington nchini Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara wa Marekani uliofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi za Chemba ya Biashara ya Marekani jijini Washington nchini Marekani.