MHESHIMIWA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ATUMA SALAMU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Salamu za Krismasi naMwaka Mpya kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan.

“Tumeanza juma la mwisho kuufunga mwaka 2023 lenye sikukuu mbili za Krismasi na Mwaka Mpya. Namuomba Mwenyezi Mungu ili sote tuweze kufikia siku hizi tukiwa wazima wa afya, kusherehekea kwa pamoja, kwa upendo, amani, furaha na usalama.

Katika sherehe hizi, baadhi yenu mnasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kujiunga na familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawasihi kuzingatia sheria ya usalama barabarani na kuchukua tahadhari na umakini mkubwa ili juma hili likawe lenye furaha, mkawe na muda mzuri na ndugu, jamaa na marafiki, na baadaye nyote mrejee mkiwa wazima wa afya kuendelea kufanya kazi ya kuliletea taifa letu maendeleo.”

MHESHIMIWA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AAPISHA VIONGOZI WATEULE NA AKUTANA NA WADAU NA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana, Kamishna wa Maadili Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Mahendeka, Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendega na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Tanzania Startup Association (TSA) ikiongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Paul Makanza pamoja na wajumbe aliofuatana nao walipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tanzania Startup Association (TSA) Ndugu Paul Makanza, Mtendaji Mkuu Ndugu Zahoro Muhaji na Makamu Mwenyekiti, Ndugu Lulu Ng’wanakilala pamoja na wajumbe waliofuatana nao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.