MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA KWA UWAZI NA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU TAIFA STARS, IKULU, JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakionesha ishara ya magoli matatu ambayo timu ya Taifa iliupata siku ya jumapili zidi ya Timu ya Taifa ya Uganda The Craines na kufanikiwa kufuzu kucheza Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON nchini Misri baadae mwaka huu.
Sehemu ya Wachezaji wa wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars Shabani Iddi Chilunda mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji hao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya Timu ya Taifa Stars ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na wachezaji Wachezaji wa wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akijitambulisha Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza kuhusiana na mafanikio yake makubwa aliyoyapata katika ngumi za kulipwa pamoja na kuitangaza nchi kimataifa.
Mfungaji wa goli la pili la Taifa Stars zidi ya Uganda Erasto Nyoni akijitambulisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akizungumza mara baada ya kupewa nafasi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Bondia Hassan Mwakinyo alipokuwa akizungumza.
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Jonas Mkude akifurahia jambo wakati wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na wachezaji wenzake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Peter Tino ambaye alifunga goli moja lililoipeleka Tanzania kwa mara ya kwanza katika michuano ya AFCON mwaka 1980 iliyofanyika nchini Nigeria. Pia Rais Dkt. Magufuli amemsaidia mchezaji huyo wa zamani kiasi cha Shilingi milioni tano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anapata chakula cha mchana na viongozi pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Rais wa TFF Walace Karia, Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo wapili kutoka kushoto katika picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
================ ===================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Machi, 2019 amekutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za michuano ya soka Barani Afrika kwa mwaka 2019 (AFCON-2019) na pia amempongeza bondia Hassan Mwakinyo ambaye juzi alishinda pambano lake dhidi ya bondia Sergio Gonzalez wa Argentina lililofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
Hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Kamisheni ya Ngumi Tanzania (TPBRC) na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na matokeo ya mchezo wa jana ambapo Taifa Stars iliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa magoli 3-0 na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wanamichezo wote kwa kuwa mafanikio yao yanaliletea Taifa sifa na heshima na pia yanatangaza fursa mbalimbali ikiwemo utalii, biashara na uwekezaji.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars, viongozi wa TFF, Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars na Watanzania wote kwa kuungana pamoja kuishangilia timu yao katika mchezo wa jana bila kujali tofauti zao za kidini, itikadi za kisiasa, makabila na kanda wanazotoka.
“Kwa kweli jana nilifurahi sana jinsi mlivyokuwa mnacheza na jinsi mlivyofunga magoli, Watanzania wanataka furaha, sio kufungwafungwa kama mlivyofungwa kule Lesotho, ile iliniuma sana hadi nilipanga kuwa sitaita tena timu kuja hapa Ikulu, lakini sasa safi.
Nataka niwahakikishie Serikali ipo na nyinyi na ni matarajio yangu kuwa mtajiandaa vizuri ili mkafanye vizuri katika michuano ya AFCON huko Misri, sasa vita imeanza” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ametoa changamoto kwa wadau wote wa michezo kuhakikisha wanasimamia uboreshaji wa miundombinu ya michezo, wanajipanga vizuri kwa michezo mbalimbali ya kuiwakilisha nchi, wanarekebisha dosari zote zilizosababisha kusuasua kwa Tanzania katika michezo ya kimataifa na ameipongeza TFF kwa kufanikiwa kurejesha mgao wa fedha za maendeleo kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Aidha, ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufuatilia uendeshaji wa uwanja wa Taifa ili kujiridhisha juu ya mapato na matumizi ya fedha za uwanja huo pamoja na kuangalia ubora wake kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa maeneo yanayoharibika hayafanyiwi matengenezo inavyopaswa.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi alioupata hapo juzi baada ya kumpiga kwa knockout bondia Sergio Gonzalez wa Argentina katika pambano lisilo la ubingwa lilifanyika Jijini Nairobi nchini Kenya, pamoja na mapambano mengine ambayo alishinda na amemtaka kuendelea kufanya vizuri katika mapambano mengine ili kuipatia sifa Tanzania.
“Nafahamu kuwa unazo changamoto nyingi ambazo hukusema hapa, lakini nakupongeza sana, juzi umemtandika yule jamaa mpaka akakaa chini na huwa nakuona unavyofanya mazoezi makali kwa kutumia matairi, wewe ni kijana safi sana” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya Serengeti Breweries Limited ambayo ni wadhamini wa timu ya Taifa Stars na SportPesa ambao ni wadhamini wa bondia Hassan Mwakinyo kwa mchango wao mkubwa wa kuendeleza michezo.
Katika hafla hiyo Mhe. Rais Magufuli amekubali maombi yaliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya kusaidiwa maandalizi ya michuano ya AFCON kwa vijana wa chini ya miaka 17 iliyopangwa kuanza tarehe 14 Aprili, 2019 hadi tarehe 28 Aprili, 2019 Jijini Dar es Salaam huku Tanzania ikiwakilishwa na timu ya Serengeti Boys, ambapo amesema Serikali itatoa shilingi Bilioni 1 kusaidia maandalizi hayo.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli ametoa zawadi ya kiwanja kimoja cha kujenga nyumba Jijini Dodoma kwa kwa kila mchezaji wa Taifa Stars, Bondia Hassan Mwakinyo, mchezaji wa zamani na Nahodha wa Taifa Stars Leodgar Tenga na mchezaji wa zamani na mfungaji wa bao lililoiwezesha Tanzania kucheza robo fainali ya AFCON mwaka 1980 Peter Tino ambaye pia amezawadiwa shilingi Milioni 5.
Kwa upande wao wachezaji wa Taifa Stars ambao wameongozwa na Nahodha Msaidizi Himid Mao na bondia Hassan Mwakinyo wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Serikali kwa ushirikiano mkubwa walioupata hadi kufikia mafanikio hayo na wamemuahidi kuendelea kufanya vizuri katika michezo inayofuata.
Rais wa TFF Bw. Wallace Karia na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Leodgar Tenga wamesema baada ya kufuzu kucheza fainali za AFCON sasa Taifa Stars inaelekeza nguvu zake kujiandaa na michuano hiyo mikubwa Barani Afrika na pia wameelezea matumaini makubwa ya Tanzania kufanya vizuri katika michuano ya AFCON kwa vijana wa chini ya miaka 17 ambapo Tanzania itawakilishwa na timu ya Serengeti Boys, michuano ya AFCON kwa wanawake ambapo Tanzania inawakilishwa na Twiga Stars na kufanya vizuri kwa timu ya Taifa ya Soka chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heros) ambayo tarehe 31 Machi, 2019 itacheza na Eritrea Mjini Asmara.
Pamoja na kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars na Bondia Hassan Mwakinyo Mhe. Rais Magufuli amekula chakula cha mchana na wachezaji hao.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Machi, 2019

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA QATAR, IKULU, JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than aliyeambatana na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kinyago Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi wanne kutoka kulia, Balozi wa Tanzania kutoka Qatar Fatma Rajab watatu kutoka kushoto pamoja na Balozi Zuhura Bundala wakwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KWA NIABA YA SERIKALI YA TANZANIA, AAGIZA KUTOA MSAADA WA CHAKULA, DAWA NA VIFAA VYA KUJIHIFADHI KWA NCHI ZILIZOFIKWA NA MAAFA YA KIMBUNGA NA MAFURIKO

Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vimewasili Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai kilichosababisha mafuriko na vifo vya watu zaidi ya 2,000 katika mji huo. Msaada huo ambao umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli umepelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ((JWTZ).

Ndege ya JWTZ ikiwa na misaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua ikiwasili Mjini Beira nchini Msumbiji

Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vimewasili Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai k
Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vikishushwa Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai

Msaada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi umewasili Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa yaliyosababishwa na kimbunga Idai ambacho kimeikumba sehemu ya nchi hiyo.

Pamoja na kusababisha mafuriko, vifo na maelfu ya kaya kukosa makazi, kimbunga hicho kimesababisha kaya nyingi kuhitaji chakula, dawa na mahali pa kujihifadhi kwa haraka.
Nchi nyingine zilizokumbwa na kimbunga hicho ni Msumbiji na Malawi ambako maelfu ya watu wamepoteza maisha na mamilioni kukosa makazi.
Jana Machi 19, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alitoa msaada wa tani 214 za chakula, Dawa tani 24 na vifaa vya kujihifadhi vikiwemo blanketi, shuka, vyandarua na magodoro ambavyo vilipelekwa katika nchi hizo kwa ndege na Malori ya Jeshi.

Msaada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi vikishushwa mjini Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa

Makabidhiano ya saada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi mjini Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa

MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA URUSI MHESHIMIWA MIKHAIL BOGDANOV KATIKA MAZUNGUMZO YA KUIMARISHA MAHUSIANO YA NCHI MBILI, IKULU, JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov kabla ya kuanza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov ambaye aliambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov zawadi ya Kinyago cha Mpingo kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov picha ya Mlima Kilimanjaro ambayo alimkabidhi kama zawadi kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Kitabu chenye Mambo ya Urusi  alichopewa zawadi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov watano kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi watano kutoka kulia, Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali mstaafu Simon Mumwi watatu kutoka kulia, Balozi Zuhura Bundala wapili kutoka kushoto pamoja na Maofisa wengine kutoka nchini Urusi Ikulu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA IKULU