SHULE YA SEKONDARI TEGETA WAANDAMANA BAADA YA KUPOTEZA MWAKA MZIMA BILA YA ELIMU

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tegeta, Dar es Salaam, waandamana kwa madai ya kupoteza mwaka mzima bila elimu na hata kulazimishwa kusomea masomo wasiyo na hamasa nayo. Je, ndiyo hawa watoto tunaowaandaa kwa taifa la baadae? Lazima tufike wakati tubadilike kifikra na tuangalie jinsi gani tuweke miundombinu ya kuhakiki shule zote za msingi na sekondari ili ziwepo kwenye tochi husika na kuhakikisha hakuna mtoto wa Kitanzania anaachwa nyuma kielimu kuelekea Tanzania mpya.

Bila ya shaka ni kazi kubwa inayofanywa na serikali kwa hivi sasa chini ya uongozi wa Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Magufuli na hasa ukiangalia serikali ya awamu ya tano inavyojitahidi kuleta mabadiliko mbalimbali katika kila sekta. Mwanzo ni mgumu na changamoto ni nyingi kama alivyosema Rais mstaafu wa awamu ya nne katika makala yake na Gulf News (bonyeza hapa), ambayo yana akisi matarajio ya mustakbali wa Tanzania kwenye nyanja ya elimu.

Nina amini tukijipanga na kuongeza bajeti kila mwaka kuwekeza kwenye sekta hii, hatutohitaji kuangalia kwingine bali kumuwezesha mtoto wa Kitanzania kwa urithi wa “ELIMU KWA WOTE” chini ya mwamvuli wa taifa moja la Mtanzania.

Je, ni kweli tupo tayari kufanya mabadiliko ya katiba kwenda na kasi ya dunia iliyoendelea wakati hatujajitayarisha ki-miundombinu ya misingi ya watoto wetu? Nini lengo hasa, na ni nini hatima yake?

Mtazamo wangu, ni mapema mno kubadili katiba kwenye ibara zote za Kijamii ikiwa hali ni hii, kwa sasa na hata hapo baadae bali matukio yapimwe kitakwimu na kwa uzito wa tukio. Kwasababu bila ya kufanya hivyo kwa sasa, athari zake hazitomgusa mtu mmoja au watu wa sehemu moja tu, bali ni taifa zima na hatimaye tutabaki “majuto mjukuu”. Narudia, kujenga kilichojengwa ni kukibomoa.

Samahani kama nimekosea popote.